Benki ya Kilimo, TPB, NMB waingia makubaliano kuwasaidia wakulima wadogo

Kaimu Mkurugenzi  wa Mikopo toka Benki ya Posta  Bw,  Ramadhan Mganga akijadiliana jambo na waandishi wa habari  makao makuu ya benki ya maendeleo yakilimo nchini (TADB) jijini Dar es salaam  mara  baada ya kumaliza kikao kilichowakutanisha  wakuu wa mikopo toka benki ya  TADB, NMB na Benki ya Posta  kuangalia namna bora  ya kuwasaidia wakulima  wadogo wadogo  kupitia Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima wadogo(SCGS). (Kushoto) kwake  ni Meneja Mfuko huo  kutoka TADB, Bw. James Mwakilima, kulia ni Meneja Masoko na Uhusiano wa TADB, Bw. Said Mkabakuli na kulia ni Meneja Mikopo  wa Benki ya Posta Bw. Mtewele Lucius.


Meneja Mfuko  wa Dhamana kwa Wakulima wa TADB, Bw. James Mwakilima (wapili kushoto) akifafanua jambo  kwa waandishi wa habari  kwenye kikao kilichowakutanisha wakuu wamikopo kutoka benki  za  TADB, NMB na  Benki ya Posta kuangalia namna bora  ya kuwasaidia wakulima  wadogo wadogo  nchini kupitia mfuko wa dhamana kwa wakulima wadogo(SCGS).  (Kulia) ni  Meneja Mikopo wa Benki ya Posta, Bw. Mtewele Lucius(kushoto) ni Meneja masoko na uhusiano toka TADB Bw. Saidi Mkabakuli (Wapili kulia) ni Kaimu Mkurugenzi  wa Mikopo wa Benki ya Posta  Bw  Ramadhan Mganga.

Meneja Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima wadogo wa TADB, Bw. James Mwakilima  (katikati) akiagana na Kaimu Mkurugenzi  wa Mikopo wa Benki ya Posta  Bw,Ramadhan Mganga mara baada ya kumalizika kikao cha kujadiliana namna bora ya kuwasaidia wakulima wadogo hapa nchini kupitia mfuko wa dhamana kwa wakulima wadogo(SCGS) jijini Dar es salaam. Kulia ni Meneja Masoko na Uhusiano wa TADB, Bw. Saidi Mkabakuli.


Na Abdallah Luambano, Dar es Salaam


Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeingia makubaliano na Benki za Biashara za NMB na Benki ya Posta (TPB) lengo likiwa kuwasaidia wakulima wadogo wadogo kupitia Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo chini ya TADB.

Makubaliano hayo yamefikiwa ili kumwezesha na kumwinua mkulima mdogo aweze kumudu kilimo chenye tija, kupunguza umaskini na kufikia malengo ya serkali ya kufikia uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao cha pamoja cha Wakuu wa Mikopo wa benki hizo tatu pamoja Meneja anayesimamia mfuko huo Jijini Dar es Salaam jana,  Meneja wa Mfuko huo, Bw. James Mwakilima alisema Serikali imeshatoa kiasi cha shilingi bilioni 45 kwa mfuko kwaajili ya  kuwakopesha wakulima wadogo  sehemu mbalimbali hapa nchini.

“Katika kutimiza azma yake ya kujenga uchumi wa kati na viwanda, Serikali imeshatoa shilingi bilioni 45 kwa TADB kupitia  mfuko  wake wa dhamana kwa wakulima wadogo ili wakulima waweze kujikita  kwenye kilimo chenye tija.” alisema Bw. Mwakilima

Bw. Mwakilima alitoa wito kwa wakulima nchini kuitumia vyema fursa hiyo kwa kuwa itakuwa fahari kubwa kwa Benki ya Kilimo kuona wakulima wanainuka kiuchumi na kufikia malengo ya serikali ya uchumi wa kati na viwanda kwa kuwa hakuna viwanda visivyo na malighafi.

“Ni nafasi pekee kwa  wakulima wadogo hapa nchini kuitumia vyema fursa hii kwani Benki ya kilimo ni moja ya madaraja ya kumvusha mkulima kutimiza malengo yake. alisisitiza Bw. Mwakilima.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya Posta (TPB),Bw. Ramadhan Mganga alisema kuwa kupitia Mfuko huo Benki yake imefanikiwa kuwakopesha wakulima wadogo hapa nchini.

“ Kupitia mfuko huu wa dhamana kwa wakulima wadogo, Benki ya Posta imeweza kuwakopesha wakulima zaidi ya shilingi bilioni 3.5 kwa kipindi cha miezi sita tu tangu tusaini makubaliano.” alisema Bw. Mganga.

Bwana Mganga alitumia nafasi hiyo  kutaja mikoa ambayo imenufaika na mikopo kuwa ni pamoja na Simiyu, Iringa na Singida ambapo shilingi bilioni 3.5 zilikopeshwa.

“Zaidi ya Bilioni 3 zimekopeshwa kwa walima katika mikoa ya Morogoro, Iringa na Singida huku tukiendelea kufanya tafiti katika mikoa mbalimbali ili tuweze kumsaidia mkulima kuinua kipato chake.” alisema Bw. Mganga

Katika kuhakikisha wakulima wananufaika na mikopo hiyo, Benki ya Posta imekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu kwa wakulima wadogo juu ya mazao gani walime na kwa wakati gani ili waweze kuwa na kilimo chenye tija

“Licha ya kutoa mikopo kupitia matawi yetu yaliyopo nchi nzima lakini pia tumekuwa na nafasi ya kutoa elimu juu ya mikopo, mazao yanayotakiwa kulimwa na wakati gani yalimwe ili yasimpe mkulima hasara.” alisema Bw. Mganga.

TADB imejipanga kuhakikisha kuwa inashirikiana na mabenki  ya biashara ili kunifanikisha azma ya serikali ya Awamu ya Tano ya kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo ikiwemo kuwainua wakulima wadogo na kuchagiza maendeleo ya sekta ya viwanda. .

Mwisho.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

NEMC warns on emptying effluent in built-up areas, flood waters

Kirenga: Kipaumbele chetu ni mkulima mdogo kupata soko la uhakika

Gold mine in Songwe wins ministerial praise for protecting environment