Kirenga: Kipaumbele chetu ni mkulima mdogo kupata soko la uhakika


 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha kuendeleza kilimo nyanda za juu kusini mwa Tanzania(SAGCOT) Bw.Geoffrey Kirenga akizungumza jambo na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam katika mahojiano maalum juu ya namna walivyojipanga kukuza na kuendeleza mnyororo wa thamani katika mazao ya kipaumbele katika ukanda wa kusini.
  Kirenga: Kipaumbele chetu ni mkulima mdogo kupata soko la uhakika
 Na Mosses Mahundi,Dar es salaam

Kituo cha Kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania (Sagcot) sasa kinaweka kipaumbele kwenye kuinua  mnyororo wa thamani wa mazao ili wakulima wadogo katika ushoroba wa kusini mwa Tanzania wapate soko la uhakika la mazao yao.

Kauli hiyo imetoliewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Sagcot, Bw.Geoffrey Kirenga, katika mahojiano maalumu  juu ya utendaji wa taasisi yao katika kipindi cha miezi tisa iliyopita.

Amesema tasisi hiyo  kwa sasa msukumo wake ni kutumia kongani zake kuongeza mnyororo wa thamani katika mazao yanayozalishwa ili wakulima washiriki wenye katika
mapinduzi ya kilimo na kilimo kiwa na tija na wakulima washuhudie wenyewe kilimo kinavyowaletea maendeleo.

Ameyataja mazao hayo kuwa ni nyanya, chai, viazi mviringo, maziwa na soya na kusema kuwa baada ya mazao kuyaongezea thamani yamepata soko la uhakika ndani na nje ya Tanzania.

“Nguvu kubwa tumeielekeza katika kuongeza thamani mazao yanayozalishwa na wakulima katika ukanda tuliokabidhiwa na taifa, maana lengo ni kumnufaisha mkulima  na shughuli zake za kilimo na  kupata maendele yeye na taifa,” ameeleza  Bw.Kirenga, ambaye anaisimamia taasisi inayoratibu ubia baina serikali ya Tanzania, wawekezaji wa nje na ndani na wadau wa maendeleo wanaoungamkono juhudi za Watanzania.

Sagcot sasa hivi imeweka nguvu zake zote kuleta mapinduzi ya kilimo katika kongani za Ihemi, Mbarali na Kilombero ambazo zinajumuisha mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe na Morogoro. Kongani za Ludewa, Rufiji na Sumbawanga bado zinafanyiwa maandalizi.

.Ameeleza kwamba taasisi yake tayari  imeunganisha wakulima wadog katika ushoroba wa kusini mwa Tanzania na wabia hao wamefikisha huduma mbali mbali kwa wakulima na kufanya uzalishaji ongezeke maradufu. Hakutoa takwimu.

“Kupitia wabia hawa tumewafikia wakulima wengi na kuwapatia huduma stahiki ikiwemo pembejeo, elimu juu ya kilimo bora, teknolojia, viuatilivu, pamoja na kuwaunganisha na masoko ya uhakika ili kuuza mazao yao,” amesema Bw.Kirenga na kufafanua kwamba mapinduzi yenye mafanikio huambatana na changamoto.

Kazi hiyo haikuwa ndogo wala nyepesi, ameeleza mtaalamu huyo wa kilimo, na kusema kuwa Sagcot ilipoanza jitihada ya kumuinua mkulima katika ushoroba huo,  changamoto kubwa ilikuwa ni kwamba wakulima wengi hawakua na elimu ya kilimo bora na matumizi sahihi ya pembejeo. Kwa hiyo mavuno yalikuwa kidogo na hafifu na mazao hayakuwa na soko.

“Kwa hiyo kazi yetu ilikuwa ni kuwatambua wabia sahihi, wadau mbalimbali wa maendeleo na kuwashawishi tushirikiane nao kuinua wakulima katika ushoroba wetu; wakakubali. Sasa tumepiga hatua, tija katika uzalishaji mazao imeongezeka, wakulima wanatuamini na wao wanajiamini; kwa hiyo tuna msingi imara wa kuchagiza ujenzi wa
viwanda. Viwanda  ni soko zuri na salama la mazao ya wakulima na ndiyo maana tunakazana  kuyaongezea thamani mazao yao,” amefafanua

Bw.Kirenga ameeleza kwamba taasisi yao inakazania kuyaongeza  thamani ikiwa ni mchango wa Sagcot kuunga mkono juhudi ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli  ya  kujenga uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025.  “Sekta ya kilimo ndio kiungo katika kuchagiza azma ya serikali kufanikiwa.”

 Mkuu wa Kongani na Maendeleo ya Ubia, Bi.Maria Ijumba, ameleza kuwa ongezeko la mazao katika ushoroba wa kusini kimsingi ni matokeo ya kutumia mbinu ya kongani.

Ameeleza kuwa suala la kuwaunganisha wakulima wadogo  na kuwafikishia huduma ili kilimo kiwe na tija kwao lilihitaji ubunifu ndiyo sababu tasisi yao ikabinu mbinu ya kongani. .

“Mfumo wa kongani umeleta mafanikio makubwa kwa taifa.  Umetusiaidia. Imewezekana  mnyororo wa thamani wa mazao ya kipaumbele kufanyiwa kazi kikamilifu na  mazao yamepata masoko ya uhakika ndani na nje  ya nchi,” ameeleza.





Comments

Popular posts from this blog

Kigamboni gets world class secondary school

TADB-supported projects for Uhuru call