Majaliwa aipongeza kampuni ya zana za kilimo ya Agricom
Na Mosses Mahundi,Bariadi
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza Kampuni ya Agricom Tanzania kwa kuwezesha upatikanaji wa zana mbalimbali za kilimo yakiwemo matrekta, mashine za kuchakata mazao hapa nchini.
“Agricom Tanzania inafanya kazi nzuri ya kuiinua sekta ya kilimo kwa kuhakikisha zana za kilimo zinapatikana kwa wakati nchini pamoja na kutoa mafunzo kwa wakulima na wadau katika sekta ya kilimo,” alisema.
Akizungumza alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye Viwanda vya Nyakabindi Mkoani Simiyu jana kabla ya kufunga Maenesho ya NaneNane, Waziri Mkuu alisema Agricom Tanzania ni mfano mzuri mwa kampuni zinazotoa mchango mzuri kwenye sekta ya kilimo.
“Tumeweza kufikia uchumi wa kati kutokana na maboresho mbalimbali yaliyofanywa na serikali kwa kuiwezesha sekta binafsi kufanya uwekezaji uliofanikisha kuongeza ajira na mapato ya serikali ,”alisema Majaliwa.
Majaliwa alisema kuwepo na kampuni za kitanzani kama Agricom Tanzania ni mfano nzuri wa kuwepo kwa sekta binafsi imara yenye uthubutu katika kuchangamkia fursa zilizopo hapa nchini kikubwa zaidi kuendelea kujenga mazingira bora ya kufanya biashara na kuvutia uwekezaji.
Aliongezea kuwa kujenga uchumi wa viwanda nchini kunategemea zaidi upatikanaji wa malighafi ambazo zinatokana na mazao, ufugaji na uvuvi hivyo ni muhimu kuhimiza uzalishaji katika sekta hizo.
Waziri Mkuu Majaliwa aliwataka wakulima kutumia zana za kisasa zinazopatikana hapa nchini ili kufanya kilimo chenye tija ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo,uvuvi na ufugaji na kupelekea uhakika wa ziada ya chakula.
“Maboresho ya mazingira ya biashara nchini imebelekea upatikanaji wa zana za kilimo kwa urahisi jambo ambalo litakuza kilimo,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa
Alisema sekta ya kilimo chini inachangia asilimia 65 ya malighafi za viwanda na hivyo tukiendelea kutumia vifaa vya kisasa vya kilimo ili kuendelea kufanya uzalishaji wenye tija.
“Sekta ya kilimo,uvuvi na mifugo inatengeneza ajira kwa asilimia 70 hivyo ni jukumu la kila mdau kuhakikisha mazingira yanakuwa wezeshi katika kuinua sekta nchini,” alisema Majaliwa
Kwa upande wake Waziri wa Kilimo,Japhet Hasunga alisema wizara yake inaendelea kushirikiana na sekta binafsi ili kuinua kilimo nchini.
“Mpaka sasa tunauhakika wa ziada ya chakula kwa mwaka hii ni kutokana na kazi nzuri inyofanywa na wakulima katika kuongeza tija ya uzalishaji,”alisema Waziri Hasunga
Maonyesho ya nanenane kitaifa yamefanyika mkoani Simiyu yakiyobeba kauli mbinu “ Kwa Maendeleo ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi chagua uongozi Bora 2020”.
Comments
Post a Comment