Viongozi wa ushirika Rukwa wapata mafunzo kutumia matrekta kuinua kilimo
Na Moses Ferdinand, Sumbawanga
Viongozi wa ushirika
Mkoani Rukwa wanapata mafunzo ili vyama vya msingi vya ushirika viweze
kusimamia kwa ufanisi matumizi ya matrekta kama ilivyoainishwa katika
mpango wa kuinua sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDPII).
Mafunzo hayo yanatolewa
kabla ya Kampuni ya Agricom Africa Company Limited kutoa matrekta
kwa vyama vya msingi vya ushirika ili kuinua uzalishaji wa mahindi katika kila
wilaya ya mkoa wa Mpanda. Kwa mujibu wa programu hii chama cha msingi chenye
wananchama wanaozidi 72 ambacho kitakuwa na fedha ya awali ya kulipia matrekta
kitapewa matrekta ili kuinua uzalishaji wa mazao na kuinua kipato cha wakulima
kama ASDP II inavyotaka.
Akizindua mafunzo
hayo hapa jana Katibu Tawala Msaidiz (Uchumi na Uzalishaji) Bw.Ocram Chengula,
ameisifu kampuni ya Agricom Africa kwamba inatekeleza kwa
vitendo programu ya ASDP II. “ASDP II imejielekeza katika kuhakikisha
matumizi ya zana bora za kilimo zinawafikia wakulima nchini ili kuongeza tija
ya uzalishaji mazao nchini. Kampuni hii ASDP II kwa vitendo,” amesema
Bw.Chengula
Amesema asilimia
kubwa ya wakulima wa Rukwa wanatumia jembe, wanyama kazi na wachache wanatumia
matrekta na kuongeza kwamba mafunzo hayo yatakuwa chachu ya kuanza
kutumia zana za kisasa katika na kuinua kilimo biashara, na kuongeza kwamba
uzinduzi wa programu hiyo utaongeza hamasa ya uzalishaji wa mazao hususani
mahindi nakuufanya mkoa kutosheleze kwa chakula na iuzwe na
kuinua kipato cha wakulima.
Mkoa wa Rukwa una
hecta 574,291 nzuri za kilimo ambazo kwa kiasi kikubwa zinamilikiwa na
wanachama wa vyama vya msingi vya ushiriaka. Kwa kawaida hekta
303,393 kila mwaka hupandwa mazao ya nafaka na mboga. Kati ya hizi hekta
1,049 ( au asilimia 0.3) hupandwa mazao wakati wa vuli na hekta 302,345 (aslimia
99.7) hupandwa mazao wakati wa masika.
Kaimu Meneja Mkuu wa
Kampuni ya Agricom Africa, Bw. Remmy Nindi, amesema kampuni yake inaelewa mkoa
wa Rukwa una fursa kubwa za uzalishaji wa mazao ya mahindi.
“Rukwa ina nafasi
kubwa ya kuzalishaji kwa wingi zao la mahindi kutokana na ardhi yake. Hivyo kwa
kuwapatia elimu ya matumizi ya zana za kisasa za kilimo kutaongeza uzalishaji
mara tatu ya walivyokuwa wakizalisha awali,” amesema Bw.Nindi. Amesema kampuni
yao ina matawi Morogoro,Mbeya,Dodoma na Kahama.
Mrajisi Msaidizi
wa Vyama vya Ushirika, Bw.Benjamin Mangwala, ofisi yake itahakikisha matumizi
sahihi ya zana za kilimo zitakazo milikiwa na vyama vya msingi vya ushirika ili
kuwaletea maendeleo wanachama wa vyama hivyo.
“Tutaandaa mwongozo
wa namna bora ya kusimamia matumizi ya zana hizi katika vyama vya ushirika ili
wanachama wake waweze kunufaika na pia iwe sehemu ya kuwaongezea kipato katika
vyama kwa kutumia zana hizo katika shughuli mbalimbali,” amesema Bw.Mangwala
Comments
Post a Comment