Benki ya Kilimo, TPB, NMB waingia makubaliano kuwasaidia wakulima wadogo
Na
Abdallah Luambano, Dar es Salaam
Benki
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeingia makubaliano na Benki za
Biashara za NMB na Benki ya Posta (TPB) lengo likiwa kuwasaidia wakulima wadogo wadogo kupitia Mfuko wa
Dhamana kwa Wakulima Wadogo chini ya
TADB.
Makubaliano
hayo yamefikiwa ili kumwezesha na kumwinua mkulima mdogo aweze kumudu
kilimo chenye tija, kupunguza umaskini na kufikia malengo ya serkali ya kufikia uchumi wa kati na viwanda
ifikapo 2025.
Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kikao cha pamoja cha Wakuu wa
Mikopo wa benki hizo tatu pamoja Meneja anayesimamia mfuko huo Jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Mfuko
huo, Bw. James Mwakilima alisema Serikali
imeshatoa kiasi cha shilingi bilioni 45 kwa mfuko kwaajili ya kuwakopesha wakulima wadogo sehemu
mbalimbali hapa nchini.
“Katika
kutimiza azma yake ya kujenga uchumi wa kati na viwanda, Serikali
imeshatoa shilingi bilioni 45 kwa TADB kupitia mfuko wake wa dhamana kwa wakulima wadogo ili wakulima waweze
kujikita kwenye kilimo chenye
tija.” alisema Bw. Mwakilima
Bw.
Mwakilima alitoa wito kwa wakulima nchini kuitumia vyema fursa hiyo kwa kuwa
itakuwa fahari kubwa kwa Benki ya Kilimo kuona wakulima wanainuka kiuchumi na kufikia malengo ya serikali ya
uchumi wa kati na viwanda kwa kuwa hakuna
viwanda visivyo na malighafi.
“Ni
nafasi pekee kwa wakulima wadogo hapa nchini kuitumia vyema fursa hii kwani
Benki ya kilimo ni moja ya madaraja ya kumvusha mkulima kutimiza malengo yake. alisisitiza Bw. Mwakilima.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya Posta (TPB),Bw. Ramadhan
Mganga alisema kuwa kupitia Mfuko huo Benki yake imefanikiwa kuwakopesha wakulima
wadogo hapa nchini.
“
Kupitia mfuko huu wa dhamana kwa wakulima wadogo, Benki ya Posta imeweza
kuwakopesha wakulima zaidi ya shilingi bilioni 3.5 kwa kipindi cha miezi sita tu tangu tusaini makubaliano.” alisema
Bw. Mganga.
Bwana
Mganga alitumia nafasi hiyo kutaja mikoa ambayo imenufaika na mikopo kuwa ni
pamoja na Simiyu, Iringa na Singida ambapo shilingi bilioni 3.5 zilikopeshwa.
“Zaidi
ya Bilioni 3 zimekopeshwa kwa walima katika mikoa ya Morogoro, Iringa na
Singida huku tukiendelea kufanya tafiti katika mikoa mbalimbali ili tuweze kumsaidia mkulima kuinua kipato
chake.” alisema Bw. Mganga
Katika
kuhakikisha wakulima wananufaika na mikopo hiyo, Benki ya Posta imekuwa mstari
wa mbele katika kutoa elimu kwa wakulima wadogo juu ya mazao gani walime na kwa wakati gani ili waweze kuwa
na kilimo chenye tija
“Licha
ya kutoa mikopo kupitia matawi yetu yaliyopo nchi nzima lakini pia tumekuwa
na nafasi ya kutoa elimu juu ya mikopo, mazao yanayotakiwa kulimwa na wakati gani yalimwe ili yasimpe mkulima hasara.” alisema Bw. Mganga.
TADB
imejipanga kuhakikisha kuwa inashirikiana na mabenki ya biashara ili
kunifanikisha azma ya serikali ya Awamu ya Tano ya kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo ikiwemo kuwainua wakulima
wadogo na kuchagiza maendeleo ya sekta ya
viwanda. .
Mwisho.
Safi sana
ReplyDelete