NEMC yahimiza ushirikiano na halmashauri kulinda mazingira, kuvutia wawekezaji


Na Abdallah Luambano,Dar es salaam

Baraza la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira nchini (NEMC) limeziomba halmashauri nchini kuweka mazingira safi na salama ili kulinda afya za watu na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje.

Mkurugenzi wa NEMC, Dkt Samuel Gwamaka,  amesema hapa kwamba mafanikio ya nchi ya kiuchumi lazima yaendane  na ustawi, usimamizi na utunzwaji wa mazingira ili kulinda afya za watu, uhai wa viumbe wengine na kuwavutia wawekezaji.

“Nchi yetu imepata mafanikio makubwa. Ili mafanikio haya yawe endelevu  lazima halmashauri zihakikishe mazingira ni rafiki kwa jamii.” Alisema Dkt. Gwamaka.

Dk. Gwamaka amesema mazingira ya  yakiwa mazuri na salama yatavutia wawekezaji wengi zaidi kutoka nje ya nchi yetu na  mapato yataongezeka kutokana na kodi na hata kuchagiza fursa za ajira kwa  vijana nchini.

“Natoa rai kwa halmashauri zetu kutambua kwamba hawa wawekezaji wanaangalia vitu vingi ikiwemo na mazingira ya eneo la kuwekeza hivyo ni jukumu letu kushirikiana kwa pamoja kuweka maeneo yetu safi ili tuwavutie wawekezaji  kuwekeza katika maeneo yetu”. Alisema Dkt. Gwamaka.

Dk. Gwamaka amesema  sasa ni wakat wa halmashauri kutambua fursa zilizomo kwenye taka, na kueleza kuwa  taka zikichambuliwa vyema zinapata soko  viwandani na kutoa mfano wa plastiki na  chuma chakavu ambayo amesema ni aina za taka ambazo hufanyiwa urejezwaji na kutumika kutengenezea bidhaa mpya.

“Tuache kuishi kimazoea. Halmashauri zetu zote ziwaongoze wananchi, na hasa vijana, wachangamkie fursa kwani taka kama vile chuma chakavu na plastiki ni aina ya taka zinazohitajika sana viwandani,” ameeleza Dk. Gwamaka.

Dk Gwamaka ametoa  mfano Halmashauri ya Jiji la Mbeya na kusema halmashauri hiyo imekuwa ikishirikiana kwa karibu sana na NEMC katika kutatua changamoto na matatizo ambayo yamekuwa yakiibuka mara kwa mara.

Elimu kwa umma ya mara kwa mara ni moja ya majukumu ya NEMC ambayo yametamkwa katika sheria ya mazingira.

 

Comments

Popular posts from this blog

Set aside land for investment, Kairuki tells RCs,district councils

Mkuu wa Mkoa Pwani asifu juhudi za mmiliki wa Makampuni ya Global Packaging na Wande Printing

17 projects to house 80,000 tonnes of crops being built