Makamba aiambia Bodi ya NEMC: komesha rushwa na vyeti feki
| Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba(kushoto) akizungumza jambo na Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Baraza la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC), Prof. Esnati Chaggu(kulia) mara baada ya kuzindua bodi hiyo jijini Dar es salaam jana. Wapili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt.Samwel Gwamaka na Wapili kulia ni Mjumbe wa Bodi Prof. Dos Santos Silayo. |
WAZIRI wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira), Bw January Makamba,
jana ameitaka bodi mpya ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kudhibiti
rushwa inayoendekezwa na
wafanyakazi na baraza na utoaji wa vyeti feki.
Akizundua bodi hiyo Jijini Dar es Salaam, Waziri Makamba
ameitaka bodi isimamie NEMC ili mchakazo wa
tathimini ya athari ya mazingira (TAM) ufanyike haraka na uwe wa ubora unaotakiwa. NEMC, ameiambia bodi,
inakabiliwa na jukumu kubwa la kupitia maandiko
ya miradi na ripoti za TAM ambazo
ni nyingi sana kwa sasa.
Waziri amesema: “Nasisitiza sana kuwa, tujitahidi kuepuka
migogoro
inayosababishwa na utoaji wa vyeti vya mazingira
katika maeneo ambayo hatimaye
yanasababisha malalamiko. Pia bodi ihakikishe matatizo ya
rushwa miongoni mwa wafanyakazi pamoja na uotaji
wa vyeti feki
hayajitokezi tena.”
hayajitokezi tena.”
Waziri huyo amekumbusha kuwa hifadhi ya mazingira siyo tu ni
agenda ya kitaifa na kimataifa
inayobadilika kwa kasi kubwa bali ni suala la kiufundi. Ameitaka bodi ihakikishe NEMC inakuwa na
wataalamu wa kutosha na wenye
ujuzi katika fani zinazotakiwa.
Ametaja changamoto zinazoendela kwa kasi kuwa mabadiliko ya tabianchi, mmomonyoko wa
utando wa tabaka la ozoni, viumbe vilivyobadilishwa vinasaba (GMOs) na kuenea kwa jangwa.
utando wa tabaka la ozoni, viumbe vilivyobadilishwa vinasaba (GMOs) na kuenea kwa jangwa.
Pia NEMC iratibu na kufanya taifiti zinazolenga kutoa
suluhisho la matatizo ya mazingira nchini, na
kuhakikisha shughuli za maendeleo zinafanyiwa
tathimini ya athari ya mazingira na unafanyika utuatiliaji.
Ametaka bodi itoe
maoni katika mchakato wa kupata sera mpya ya
mazingira inayofikiriwa.
Ametaka bodi ilisaidie baraza kupanua wigo wa mapato kwani, amesema, sasa hivi vyanzo vya makusanyo ni vichache ikilinganishwa na vile vilivyopo kisheria. NEMC inajiendesha kutokana na mapato yake.
Ametaka bodi ilisaidie baraza kupanua wigo wa mapato kwani, amesema, sasa hivi vyanzo vya makusanyo ni vichache ikilinganishwa na vile vilivyopo kisheria. NEMC inajiendesha kutokana na mapato yake.
Ametaka NEMC ianzishe kanda ya magharibi ili iwe na kanda
saba.
Waziri amegusia uhaba wa utaalamu katika fani za
gesi, mafuta na madini na kuitaka
bodi isimamie baraza kujenga uwezo wa kukabiliana na changamoto hii na zingine. Sasa hivi NEMC ina
wafanyakazi 150.
Amekumbusha kwamba mafanikio ya NEMC katika
utekelezaji wa shughuli za hifadhi ya mazingira unatemea
sana uwezo na uelewa wa wadau ambao sasa
hivi ni mdogo. Ameitaka bodi ihakikishe NEMC inaendeleza juhudi
ya kujenga uwelewa wa wadau ili washiriki vizuri
katika kuhifadhi mazingira.
Mwenyekiti wa Bodi, Profesa Esnati Osinde Chaggu ameahidi kwamba utakuwepo ushirikiano baina ya bodi, NEMC, wizara na wadau.
Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt Samuel Gwamaka Mafwenga, ameahidi mabadiliko makubwa ya kiutendaji na kusema baraza litapambana na
wanaoendesha shughuli za kibinadamu katika
vyanzo vya maji.
“Tutasimamia sheria na kanuni za mazingira bila woga wala upendeleo kwa mtu au taasisi yeyote,”alisema Dkt. Gwamaka na kuahidi kufanya kazi kwa karibu sana na bodi pamoja na timu ya mejimenti.
Mbali ya Prof. Chaggu, wajumbe wengine waliopo kwenye Bodi hiyo iliyoteuliwa hivi karibuni na Rais Magufuli ni Dkt. Flora Tibarazwa,
Prof. Hussein Sosovele, Dkt. Catherine Masao,
Bw. Damas Masologo, Dkt. Neduvoto
Mollel, Prof. Dos Santos Silayo, Dkt. Mwakalukwa Ezekiel na
Prof. William Mwegoha.
Prof. William Mwegoha.
Mwisho.
Comments
Post a Comment