NEMC yahimiza uhifadhi wa mti wa msandali

NEMC yahimiza uhifadhi wa mti wa msandali
Na Mwandishi wetu,Manyara
Baraza la Taifa la Uhifadhi wa Usimamizi wa Mazingira(NEMC) limetoa wito kwa watanzania kujikita katika upandaji wa miti ya misandali kwa lugha ya kitaalum ‘Osyris lanceolata’ ikiwa ni sehemu ya kutunza mazingira na pia fursa ya biashara kutokana na umuhimu wa miti hiyo katika kuzalisha bidhaa mbalimbali.
Akizungumza na waandashi wa habari mara baada ya kutembelea kiwanda cha kuzalisha mafuta  ya kutengenezea manukato cha Sierra limited kilichopo mkoani Manyara, Mwenyekiti wa Bodi ya NEMC, Prof.Esnat Chaggu alisema kunaumihimu kubwa wa kupamba miti ya aina tofauti tofauti kutokana na faida zake kimazingira na kiuchumi pia.
“Hii ni fursa kwa vijana kujikita katika kupanda mashamba ya miti ya misandali ambayo faida yake kwa baade ni kubwa kutokana na uhitaji mkubwa wa mti huo katika kuzalisha malighafi ya kutengenezea manukato,” alisema Prof.Chaggu
Alisema uwekezaji wa aina hii kwa vijana unawaletea faida kubwa kiuchumi mara baada ya kuivuna na pia mazingira yatakuwa yanaendelea kulindwa hali ambayo itapelekea ustawi wa nchi kimazingira kuimalika na pia kiuchumi.
“Ni muhimu kuhamasisha watanzania nchini kupata mti wa msandali na aina nyinginezo ambayo inafaida kubwa katika matumizi yake, kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaendelea kuongeza idadi ya miti hii kuwa mingi nchini,” alisema Prof.Chaggu
Aiongezea kuwa  tafiti zinaonyesha kupungua kwa mti huu kutokana na umuhimu wake mkubwa katika kutengeneza dawa za maradhi mbalimbali kwa binadamu na pia kutengeneza mafuta yanayotumika kuzalisha manukato hivyo kama wadau wa mazaingira wanalazimika kuhamasisha upandaji wa miti hii ili kuiendeleza na kuja kusaidia vivazi vijavyo.
“Nchi yetu ina maeneo mengi ambayo tunaweza kupanda miti ya aina ya msandali kwa lengo la kuongeza idadi ya miti hiyo nchini na pia kuwa sehemu ya fursa kwa vijana kujipatia kipato kupitia uwekezaji wa miti,” alisema
Kwa upande wake Meneja wa Kiwanda cha Sierra, Bw.Ashish Upadhaye alisema mti wa msandali una matumizi mengi hasa katika afya ya binadamu hivyo ni muhimu kama nchi kuweka kipaumbele katika kulinda miti ya aina hii na pia kuhamasisha upandi wa miti hii ili iongezeke ambapo italeta faida kubwa ikitumika kama malighafi ya kuzalisha bidhaa.
“sisi ni wazalishaji wa mafuta ya msandali yanatumika katika kutengeneza dawa ya maradhi mbalimbali kwa binadamu na manukato, hivyo ni muhimu kuupa kipaumbele mti huu na miti yenye sifa kama hizi kuendelea kupandwa nchini kwa faida ya baadae,” alisema Bw.Upadhaye
Naye Mjumbe wa Bodi ya NEMC, Dkt. Neduvoto Mollel alisema faida za mti wa msandali ni nyingi hivyo wajibu wetu kama Baraza ni kusimamia zaidi katika uhifadhi wa miti ya aina hii kote nchini na pia kuhamasisha upandaji wa miti hii ili izidi kuongeza.
“imani yangu kuwa uhamasishaji ukifanyika miti mingi itapandwa nchini na kupelekea kuwa na akiba kubwa ya miti ya msandali ambayo  inafaida kubwa na muhimu kwa afya ya binadamu,” alisema Dkt.Mollel
Bodi ikiongozwa Mwenyekiti wake pamoja na watendaji NEMC wamefanya ziara katika mikoa ya Arusha na Manyara ili kujionea hali ya uhifadhi wa mazingira ilivyo katika maeneo mbali mbali kwenye mikoa hiyo na hatua za kuchukua katika kufanya usimamizi ili mazingira yabaki kuwa salama.
 Mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

Tanzania praised for being keen on fertilisers going to farmers

Gold mine in Songwe wins ministerial praise for protecting environment

NEMC warns on emptying effluent in built-up areas, flood waters