TBS yasisitiza bidhaa kuthibitishwa kabla ya kuingia sokoni



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewataka wazalishaji na watoahuduma nchini kuzingatia umuhimu wa kuthibitisha ubora wa bidhaa namfumo wa uzalishaji ili kuendana na kasi ya Tanzania ya viwanda.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Profesa Egid Mubofu  ametoa wito katika hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi Upimaji na Ugezi  waShirika hilo, Bi. Agness Mneney katika hafla ya kutunuku vyeti vimetolewa baada ya bidhaa husika au mfumo wa uzalishaji kukidhi

viwango  tayari kuingia katika ushindani wa soko.


Akizungumza mwisho mwa wiki, Bi. Mneney alisema TBS imejipanga kuwasaidia wazalishaji na watoa huduma kufikia viwango vinavyotambulika kimataifa na hivyo kutoa mchango mkubwa katika ujenziwa uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025.


 “Bidhaa hizi zitapata fursa muhimu ya kupenya katika soko la nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambako kwa makubaliano maalumu alma yetu ya ubora ‘TBS Standard Mark’ inatambulika. Hivyo nawashauri kuwajuhudi hizi za kupima bidhaa zenu ziwe endelevu,” alisema Bi. Mneney.


Kwa mujibu wa Bi Mneney, katika hafla hiyo ya kutunuku leseni zakutumia alama ya ubora, vyeti vya ubora na vyeti vya kuthibitisha mifumo ya uzalishaji, jumla ya leseni 78, vyeti vya ubora 11 na cheti kimoja cha mifumo ya uzalishaji na usindikaji salama wa chakula

vimetolewa.

“Maana yake ni kuwa siku ya leo bidhaa mpya  bora 87 kutoka viwandambalimbali vikiwemo vya usindikaji wa vyakula, mitambo, umeme,kemikali, vinywaji, vifaa vya ujenzi na vifungashio zimeongezeka katika soko la Tanzania,” alisema Bi. Mneney.

Mmoja wa wamiliki wa viwanda waliohudhuria katika hafla hiyo, Bwana Shanif Mansoor ambaye ni Murugenzi wa kampuni ya kuzalisha sigara ainaya Malboro, Mansoor Industries ya jijini Dar es Salaam alisema anaishukuru TBS kwa namna wanavyofanya kazi kwa ufanisi na wakati.“Kwa kasi hii wanayoionyesha TBS hakika Tanzania ya viwanda itafikiwa hata kabla ya mwaka 2025. Kwa sababu nilileta maombi ya kuzalishabidhaa hii ya Malboro lakini mwaka huu mchakato ukaanza na walikujakutembelea eneo la uzalishaji na mwezi wa 11 nimepata leseni,” alisema Bw. Mansoor.

Alibainisha kuwa kasi hii ya TBS katika kusaidia viwanda vya ndani na wajasiriamali wadogo, itasaidia ndani ya muda mfupi Tanzania kuwa naviwanda vingi kutokana na kuvijengea uwezo viwanda kuona fursa ya kupeleka bidhaa nje ya nchi.


Kwa upande wake mjasiriamali pekee aliyepata cheti cha mifumo ya uzalishaji salama wa chakula yaani ‘Hazard Analysis Critical Control Point (HACCP), Bwana Atanas Mluki ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Afrilife Product Ltd inayosindika asali alisema TBS imemsaidia kukua baada ya kumuingiza katika utaratibu wa kusaidia wajasiriamali wadogo.


“Nilipoanza biashara ya usindikaji asali nikiwa Shinyanga sikujua chochote kuhusiana na masuala ya ubora wa bidhaa, nilikwenda SIDO wakaniunganisha na TBS nikawa katika utaratibu wa kusaidiwa, awali ilipopimwa bidhaa yangu mara mbili ilionyesha haijakidhi viwango lakini sikukata tama hadi mara ya tatu ilipothibitisha inafaa kuingia sokoni ndipo nikapewa cheti,” alisema Bw. Mluki.


TBS imejiwekea utaratibu wa kuandaa hafla za namna hii mara kwa mara kwa lengo la kuwakabidhi vyeti wazalishaji mbalimbali ambao wameanza biashara na wale waliobadili majina pamoja na wale waliofanyiwa uchunguzi wa bidhaa kwa mara nyingine, kwa mujibu wa TBS mzalishaji anapopewa cheti ataendelea kufuatiliwa kila inapohitajika.
Baadhi ya wazalishaji kutoka viwanda 89 vipya Tanzania  wakiwa  kwenye  hafla ya kutunukiwa vyeti kwa   bidhaa ambazo zimekidhi   matakwa na taratibu  pamoja na viwango sitahiki   vyaubora wa bidhaa   iliyofanyika kwenye  ofisi   za tbs   Jijini Dar essalaam mwishoni mwa wiki.

Mkurugenzi  upimaji ,  Ugezi  na Huduma ya Ufungashaji(Testing and Calibration) Bi, AgnessMneney aliyemwakilisha  Mkurugenzi Mkuu,Profesa  Egid Mubofu akimkabidhi Cheti Mkurugenzi Mtendaji   wa Kiwanda cha Mansoor Industries Limited kinacho jihusisha na uzalishaji mafuta  ya moil pamoja na sigara aina ya Malboro, Bw. Shanif Hirani kwenye hafla ya kukabidhi vyeti wazalishaji   89 kutoka Viwanda mbalimbali   vipya iliyo fanyika  kwenye ofisi  za TBS   Jijini Dar essalaam mwishoni mwa wiki.
 Mkurugenzi  Upimaji ,  Ugezi  na Huduma yaufungashaji(Testing and Calibration) Bi, Agness Mneney ( katikati) ambaye alimwakilisha  Mkurugenzi Mkuu  (TBS) Profesa Mubofu, akisisitiza  jambo  wakati wa hafla ya kuwatunuku  vyeti wazalishaji kutoka viwanda mbalimbali 89  vipya   Tanzania  ambao   bidhaa zao zimekidhi  taratibu  pamoja na viwango sitahiki  iliyo fanyika kwenyeofisi   za TBS Jijini Dar es salaam (kushoto ) ni Mkurugenzi  waUdhibiti Ubora  Eng, Tumaini Mtitu.

Comments

Popular posts from this blog

Tanzania praised for being keen on fertilisers going to farmers

Gold mine in Songwe wins ministerial praise for protecting environment

NEMC warns on emptying effluent in built-up areas, flood waters