Chuo cha Diplomasia chaanzisha kosi ya diplomasia ya uchumi kuchochea viwanda
Msajili wa kituo cha Diplomasia na Uhusiano wa
Kimataifa (CFR), Dkt. Ally Masabo, kushoto akikagua eneo la
mradi wa ujenzi wa maktaba ya kisasa,hosteli
na vyumba vya semina na kufundishia unaendelea kituoni hapo, ambapo mpaka sasa serikali imeshatoa
takribani shilingi bilioni 12 kwaajili
ya ujenzi huo, Kulia ni Mhandisi,Athuman Mashaka.
|
Na Abdallah Luambano, Dar es Salaam
CHUO cha Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa (CFR) cha Jijini Dar es Salaam, kimeanzisha kozi ya diplomasia ya uchumi kwa wahitimu wa vyuo vikuu ili kunyanyua na kuimarisha uwezo wa majadiliano katika masuala ya uchumi, hasa ya kimataifa, wa wafanyakazi katika balozi za Tanzania na watendaji katika sekta binafsi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, Kaimu Mkurugenzi wa chuo hicho, Dkt. Jeremia Ponera, amesema mafunzo haya yanaandaa wataalamu wa Tanzania kushiriki vizuri na kikamilifu katika utekelezaji wa azma ya taifa ya kujenga uchumi wa kati na wa viwanda ifikapo 2025.
“Kituo hiki, kama taasisi nyingine za umma, tumekuwa mstari wa mbele katika kutafsiri na kuunga mkono jitihada za serikali. Katika kipindi hiki ambacho serikali imeazimia kujenga uchumi wa viwanda ifikapo 2025, kituo kinawaandaa wataalamu ambao watasaidia kueleza fursa zilizopo kimataifa ili kufikia azma hiyo kwa haraka,’’ amesema Dkt. Ponera.
Amesema Chuo hicho kimeisaidia Tanzania kuwaandaa mabalozi, wafanyabiashara za kimataifa katika kutambua fursa na kufanya majadiliano yenye tija kwa taifa. Chuo pia kimewasaidi mabalozi na wafanyabiashara kutambua umuhumu wa uwekezaji na kueleza fursa zilizopo Tanzania.
"Kama taasisi tupo katika nafasi nzuri ya kufanikisha azma ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuleta mageuzi katika ujenzi wa uchumi wa kati na viwanda," alisema Dkt. Ponera na kuongeza kuwa kila mtanzania anapaswa kuunga mkono juhudi hizo kwa vitendo.
“Mbali ya kujikita katika kutafsiri malengo ya serikali kulingana na nyakati zilizopo, Chuo kimefanya kazi kubwa katika kuwaandaa Mabalozi ambao ni wawakilishi muhimu kimataifa. Lakini pia tumekuwa na kozi fupi za kuwaandaa wafanyabiashara za kimataifa pamoja na kuonesha fursa zilizopo kwa wawekezaji wa kigeni hapa nchini,’’ ameeleza.
Aidha amesema kuwa chuo kimetengeneza programu mpya zinazojielekeza katika ujenzi wa uchumi wilayani na mikoani ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa ndani na hivyo kufikiwa kwa azma ya uchumi wa viwanda.
“Chuo hakijishughulishi tu na masuala ya kimataifa, bali hata ndani ya nchi ambapo programu mbalimbali zinazojielekeza katika ujenzi wa uchumi kwenye maeneo ya wilaya na mikoa kwa kuwa diplomasia ya uchumi inahusu namna ya kuongeza biashara za ndani na nje na kuangazia maeneo muhimu ya kiuwekezaji,’’ alieleza
Msajili wa Chuo, Dkt. Ally Masabo, ametoa wito kwa Watanzania kujiunga na chuo hicho hasa katika kipindi hiki ambacho diplomasia ya uchumi imekuwa dhana muhimu katika kujenga chumi za mataifa mbali mbali.
“Chuo cha Diplomasia kinatoa kozi za muda mfupi na muda mrefu ambazo zimejikita katika kuwajenga Watanzania kujua fursa zilizopo kimataifa ili wazitumie katika kuchochea maendeleo ya ndani ya nchi. Natoa wito kwa Watanzania kujiunga na chuo hiki,’’ amesema na kuongeza kuwa sifa za waombaji ni kuanzia wahitimu wa darasa la saba, wahitimu wa cheti, kidato cha nne na kidato cha sita.
Chuo cha Diplomasia kimeanzishwa mwaka 1978 na kinaendeshwa kwa ubia baina ya serikali ya Tanzania na Msumbiji. Chuo kina jukumu la kutoa mafunzo ya diplomasia, stretejia pamoja na lugha.

Comments
Post a Comment