Waziri Mkuu azindua mpango wa ugawaji wa mbolea bure kwa wakulima 83,000 nchini

Balozi wa Norway Nchini Bi.Elisabeth Jocobsen(wapili kulia) akizunguma jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa(wapili kushoto) mara baada ya kuzindua mpango wa kusambaza mbolea bure kwa wakulima wadogo nchini mpango umeratibiwa na Kampuni ya YARA Tanzania kupitia mradi wa uitwao Action Africa ambapo zaidi ya tani 12,500 zitatolewa. kushoto ni Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga na Kulia ni Mkurugenzi wa YARA Tanzania Winstone Odhiambo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza jambo katika uzinduzi wa rasmi wa ugawaji wa mbolea bure kwa wakulima zaidi ya 83,000 nchini uliofanyika ofisi za kampuni ya YARA Tanzania jijini Dar es Salaam na kumeratibiwa na Kampuni hiyo kupitia mradi wa Action Africa ambapo zaidi ya tani 12,500 zitatolewa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa(watatu kulia) akinyanyua bendera kuashiria uzinduzi rasmi wa ugawaji wa mbolea bure kwa wakulima wadogo nchini uliofanyika ofisi za kampuni ya YARA Tanzania jijini Dar es Salaam na kumeratibiwa na Kampuni hiyo kupitia mradi wa Action Africa ambapo zaidi ya tani 12,500 zitatolewa. Wapili kulia ni Balozi wa Norway Nchini Bi.Elisabeth Jacobsen na Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yara Tanzania Winstone Odhiambo.

 

Na Moses Ferdinand, Dar es salaam

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza watendaji wa Serikali kuhakikisha mbolea ya bure inayotolewa na kampuni ya YARA Tanzania inawafikia wakulima waliolengwa na mpango huo  kwa wakati ili kwenda sambamba na maandalizi ya msimu wa kilimo mwaka 2020/2021.

Akizindua mpango  huo wa ugawaji mbolea tami 12,500  iliyotolewa na kampuni ya YARA jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha kuwa  sekta ya kilimo inapiga hatua na kutoa mchango stahiki katika kuinua uchumi na kuongeza kipato cha mkulima mmoja mmoja hapa nchini.

“Nachukua fursa hii kuipongeza kampuni ya YARA kwa kujitoa kwake 
kuchangia kwenye kukuza sekta ya kilimo kwa kutoa mbolea bure kwa wakulima zaidi 83,000,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Alisema ni muhimu watenda wa serikali wakashirikiana na kampuni ya YARA kutimiza lengo la kuwafikishia mbolea wakulima kwa wakati na bure kama ilivyopangwa.

“Watendaji wasiwe kikwazo katika utekelezaji wa mpango huu ambao unalengo la kuwanufaisha hasa wakulima wadogo ili kuongeza uzalishaji wa mazao nchini.

Aidha, ametoa wito kwa makamuni mengine yanayojihusisha na sekta ya kilimo kuiga mfano huu wa YARA kuboresha sekta kwa kuondoa changamoto zinazowakabili wakulima.

“Natumia nafasi kuyataka kampuni mengine kujitoa ili kusaidia sekta hususani kwenye swala la pembejeo na zana za kilimo kwa kuwa kilimo ni sekta inayoajiri zaidi ya asilimia 75 ya watanzania,” alisema Majaliwa

Kwa upande wake Waziri wa Kilimo Bw.Japhet Hasunga alisema wizara yake pamoja na mamlaka za uthibiti zimejiridhisha kuwa mbolea ya YARA inafaa kwa matumizi kulingana na mazingira ya nchi yalivyo na hivyo itachochea kuongeza uzalishaji wa mazao ya mahindi na mpunga.

“Taratibu za kufanya ithibati ya mbolea hii zimezingatiwa hivyo tunaimani zitachangia katika kuongeza ubira na uzalishaji wa mazao nchini,” alisema Hasunga

Alisema Serikali itaendelea kwa kuhamasisha na kuhakikisha wakulima wanapata elimu ya matumizi ya mbolea na mbegu bora na viua tirifu zinavyofaa kulingana na ardhi yetu ili kuongeza uzalishaji ili nchi ijitosheleze kwa chakula.

“Serikali imejipanga kuhakikisha masoko ya mazao yanapatikana ili mkulima aweze kufaidika na shughuli yake jambo litakalo chochea ukuaji wa uchumi na maendeleo kwa ujumla,” alisema Hasunga

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya YARA Tanzania,Bw.Winstone Odhiambo alisema mpango huu ni jitihada za kampuni mama kutoka Norway kuhakikisha nchi za Afrika ikiwemo Tanzania zinajitosheleza kuzalisha chakula.

“Mpango huu wa usambazaji mbolea bure unafanyika kupitia mradi maalum ujulikano kama ‘Action Africa’, “ alisema Odhiambo na kuwataka wakulima hapa nchini kuchangamkia fursa hiyo kugawiwa mbolea bure.

Aina za Mbolea zinazosambazwa na kampuni ya YARA Tanzania ni NPK ambapo zaidi ya MT 12,500 zitatolewa kwa wakulima wadogo kote nchini kwa kujisajili kupitia namba *149*46*16#.





Comments

Popular posts from this blog

Set aside land for investment, Kairuki tells RCs,district councils

Mkuu wa Mkoa Pwani asifu juhudi za mmiliki wa Makampuni ya Global Packaging na Wande Printing

17 projects to house 80,000 tonnes of crops being built