Mbenna ateuliwa kaimu mkurugenzi mtendaji sekta binafsi


Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzani (TPSF) ,Bw. Godfrey Simbeye(kushoto) akiagana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Bw. Zacky Mbenna(Kulia) muda mfupi mara baada ya kufanya makabidhiano ya ofisi Jijini Dar es Salaam jana


Na Mosses Ferdinand, Dar es salaam

BODI ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzani (TPSF) imemteua Bw. Zacky Mbenna kuwa kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo rasmin kuanzia tarehe 15, Julai mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Taasisi hiyo jana na kusainiwa na Mwenyekiti wake, Bi. Angelina Ngalula, kabla ya uteuzi huo, Bw. Mbenna ambaye ni mzoefu katika masuala ya usimamizi wa biashara na utawala alikuwa Mkurugenzi wa Huduma ya wananchma wa Taasisi hiyo. 
 
Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ilisema kuwa uteuzi huo umefanywa kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji,Bw. Godfrey Simbeye ambaye amehudumu kwenye Taasisi hiyo kwa zaidi ya miaka 10.

“Kwa mara nyingine tena, Bodi ya Wakurugenzi inapenda kumshukuru Bw. Simbeye kwa kujitoa kwake katika kuhamasisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa sekta binafsi hapa nchini,” alisema Bi. Ngalula katika taarifa yake.

Bi. Ngalula amewahakikishia wanachama wote, Serikali, Wabia wa Maendeleo kuwa katika kipindi hiki cha mpito, mamlaka na shughuli za Taasisi zitaendelea kama kawaidi pasipo kuathirika.

​ TPSF ni mbia mkubwa wa serikali na wadau wengine katika kuandaa na kutekeleza sera na mikakati inayolenga kuchochea ukuajiaji na maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Tanzania.

Taasisi hiyo pia ni Sauti ya Sekta Binafsi na Mwamvuli wa vyama na mashirika katika sekta binafsi kwenye sekta za kiuchumi nchini.

Comments

Popular posts from this blog

Mbeya agro-processors get 5 acres to build 50 industries

Tanzania praised for being keen on fertilisers going to farmers

Gold mine in Songwe wins ministerial praise for protecting environment