Majaliwa aitaka YARA kuongeza uwekezaji katika sekta ya kilimo..

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza katika mkutano na wadau wa sekta ya kilimo ambapo ameipongeza kampuni ya YARA Tanzania kwa uwekezaji mkubwa wanaofanya katika sekta ya kilimo hapa Nchini,kulia ni Balozi wa Norway Nchini Tanzania, Elisabeth Jacobsen,Katikati,Mkurugenzi Mtendaji wa YARA Tanzania,Bw. Winstone Odhiambo. 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya YARA Tanzania Bw. Winstone Odhiambo (Kulia) kuhusu uwekezaji uliofanywa na Kampuni hiyo katika sekta ya kilimo, Wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Temeke, Bw. Godwin Gondwe

 

 Na Mosses Ferdinand, Dar es Salaam

WAZIRI  Mkuu  Kassim Mjaliwa ameitaka Kampuni ya mbolea bolea ya  YARA kuongeza uwekezaji wa mbolea hapa nchini sambamba na kuinua sekta ya kilimo ili  kuongeza tija  na manufaa zaidi kwa mkulima.

Akizungumza  mara baada ya kutembelea  Makao Makuu ya kampuni ya YARA yaliyopo jijini Dar es Salaam juzi pamoja mambo mengine  Bw. Majaliwa alipongeza uwekezaji uliofanywa na Kampuni hiyo sambamba  na kutaka uwekezaji zaidi kwenye sekta ya kilimo ambayi inaajiri zaidi ya asilimia 70 ya watanzania.

“Serikali ya awamu ya Tano chini ya  Rais Dkt. John Pombe Magufuli imeweka kipaumbele kwenye sekta ya kilimo  ili kuwa na  uhakika wa malighafi viwandani  na kufanikisha azma yake ya ujenzi wa uchumi wa viwanda. Tunawapongeza YARA na wadau wengine kwa namna wanavyounga mkono juhudi hizi za serikali,’’ alisema waziri mkuu.

Alifurahishwa na  juhudi za  Kampuni ya YARA ya kuwasaidia wakulima wadogo nchini katika kupunguza tatizo la ajira, kuinua sekta ya kilimo na kuhakikisha usalama wa chakula unakuwepo pamoja na kuchangia pato la Taifa.

“Tunapohimiza uwekezaji ni miongoni mwa hatua stahidi  za kuondokana na changamoto za ajira, kuinua uchumi sambamba na kuongeza pato la taifa  na kujiwekea usalama wa chakula.Tunahitaji zaidi kuongeza uzalishaji wa mazao ,’’ alieleza Waziri Mkuu.

Aidha, Bw. Majaliwa alichukua fursa hiyo pia kuwahakikishia wawekezaji hapa nchini kuwa serikali itaendelea kutatua changamoto zilizopo katika uwekezaji ili kuvutia uwekezaji zaidi katika mbalimbali za uchumi.

“Tumeona namna YARA mnavyofanya kazi zenu  katika mikoa ya  Dar es Salaam, Iringa, Mbeya, Tabora, Njombe na Kilimanjaro. Serikali itaendelea kushirikiana nanyi kwa kuweka mazingira rafiki na wezeshi ili kuwafikia wakulima wengi zaidi,” alisema.

Kwa upande wake Balozi wa Norway hapa nchini, Bi. Elisabeth Jacobsen alisema nchi yake imekuwa mstari wa mbele  kuunga mkono maendeleo ya sekta ya kilimo Barani Afrika ikiwemo Tanzania.

“Afrika imekuwa na changamoto ya upatikanaji wa chakula, YARA imekuwa na mipango mingi katika kuhakikisha panakuwepo na usalama wa chakula ikiwepo programu ya “Action Africa’’ ambayo imelenga kugawa mbolea bure ili kuwainua wakulima wadogo hasa katika kipindi ambacho ugonjwa wa corona umeathiri nchi  nyingi duniani,’’ alisema Balozi Jacobsen.

Naye Mkrugenzi Mtendaji wa Kampuni ya YARA Tanzania, Bw. Winstone Odhiambo alisema kampuni yake itaendelea kusimamia ubora wa mbolea ili kuongeza uzalishaji wa mazao  hapa nchini sambamba  kutengeneza ajira kwa watanzania.

“YARA tutaendelea kutengeneza mbolea bora ili kuzidi kumnufaisha mkulima lakini kuzidi kutoa ajira ambapo mpaka sasa tumetengeneza ajira rasmi zaidi ya 60 na ajira zisizo za kudumu zaidi ya 300,’’ alisema Bw. Odhiambo.

Hivi karibuni YARA walizindua programu ya “Action Africa” katika mikoa ya Tabora, Kigoma na Songwe ambao unalenga   kugawa  mbolea bure  kwa wakulima zaidi ya 83,000 wanatarajia kunufaika na mpango huo kwa msimu wa 2020/21.

 

 

 

 

 

Comments

  1. babyliss pro nano titanium hair dryer - Titanium Arts
    All Natural Shave Gives a Quality, and trekz titanium pairing Quality titanium nose hoop Look at Babyliss Pro trekz titanium for Men's titanium vs ceramic Shaves, titanium easy flux 125 amp welder Beard & Beyond. These products are available on our store in Colorado $49.99 · ‎In stock

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Set aside land for investment, Kairuki tells RCs,district councils

Mkuu wa Mkoa Pwani asifu juhudi za mmiliki wa Makampuni ya Global Packaging na Wande Printing

17 projects to house 80,000 tonnes of crops being built