Tanzania yajenga masailo na maghala kupambana na upotevu wa mazao
Na Abdallah Luambano, Dar es Salaam
Katika
kupambana na upotevu wa mazao baada ya mavuno unaokadiriwa kuigharimu
Tanzania hasara ya bilioni 3.92 au dola za Marekani milioni 1.8 Tanzania
inajenga masailo matono na maghala 12 ili kuhifadhi tani 80,000 za
mazao. Kati ya jumla ya tani hizi tani 34,000 zitakuwa ni za mahindi.
Nyaraka ya kitaalam iliyopatikana Jijini Dar es Salaam leo inaeleza kwamba Serikali ya
Tanzania inawakilishwa katika mradi huu mkubwa na Benki ya Kilimo ya
Tanzania (TADB).
Makadirio
ya kitaalamu yanaonyesha kwamba kila mwaka wa mavuno Tanzania hupoteza
kati ya 30% na 40% ya nafaka zinazozalishwa nchini na asilimia ya
upotevu inakuwa kubwa zaidi kwa mazao teke.
Nyaraka ya kitaalam inaeleza kwamba kadri wakulima wanavyotumia zana duni, ndiyo
upotevu wa mazao unavyokuwa mkubwa na kwamba kadri kilimo kinavyokuwa
cha mashine ndivyo upotevu wa mazao unavyopungua.
Aidha Nyaraka ya kitaalam inafafanua kuwa kwa desturi upotevu unatokea wakati wa kuanika, kuhifadhi na kuchakata mazao.
Nyaraka ya kitaalam inaeleza kuwa imekuwepo haja ya muda mrefu ya wakulima kupata
tekinolojia za kisasa, mfano wa masailo na mabohari ya kileo ili
kupambana na upotevu wa mazao baada ya kuvuna. Mradi mahususi, inasema
kumbukumbu, unatekelezwa kwa lengo hilo.
Kilimo
kinajulikana kuwa kinachangia asilimia 40 za pato la taifa (GDP) na
asimilia 58 ya wananchi wanaajiriwa na shughuli tofauti katika sekta ya
kilimo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine alipoulizwa juu ya mradi huo
ameeleza kwamba TADB inaona fahari kuwa moja ya taasisi zinazotekeleza
mradi huo kwa sababu jukumu lake la kitaifa ni kuifanya sekta ya kilimo
kuwa ya kisasa na kuboresha maisha ya wakulima, wafugaji na wavuvi.
Comments
Post a Comment