NEMC yajivunia ushirikiano wake na vyombo vya habari

Na Abdallah Luambano, Dar es Salaam 
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)limesema linajivunia ushirikiano wake na vyombo vya habari na kusema vyombo hivyo vimesaidia kusambaza elimu ya mazingira ambayo imeongeza uelewa wa wananchi juu ya umuhimu wa kuyatunza na kuhifadhi mazingira.

Akizungumza katika hafla ya utunzaji wa mazingira hapa Jijini, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk Samuel Gwamaka, elimu ya mazingira imekuwa ikitolewa na wafanyakiazi wa NEMC na taasisi nyininge zikiwemo shule na vyuo.

“Sisi kama baraza tumetoa elimu ya mazingira kwa jamii lakini pia elimu hii inatolewa hata mashuleni na vyuoni jambo ambalo linasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza uelewa kwa watu wengi,”amesema Dk Gwamaka.

Dk. Gwamaka amesema Baraza hilo linashirikiana vyema na vyombo vya habari. Aidha NEMC hutoa vipeperushi ambavyo vinahimiza utunzwaji wa mazingira.

“Nataka nikiri hapa kwamba baraza tumekua wadau wakubwa wa vyombo vya habari. Natumia nafasi hii kuvishukuru vyombo vya habari kwa kazi kubwa ya kuwaelimisha watu juu ya umuhimu wa kutunza na kuhifadhi mazingira nchini”amesema Dkt. Gwamaka.

Aidha, Dk Gwamaka amewaomba wananchi kuyaenzi mazingira na kueleza kwamba kwa kuwa Tanzania sasa ina  uchumi wa kati ni muhimu  wananchi wakayalinda mazingira yanayowazunguka kwa sababu uzalishaji katika kila sekta ya uchumi utaongezeka.

“Nchi yetu chini ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli imefikia uchumi wa kati.  Mafanikio haya ni vyema yaambatane  na kuyaenzi mazingira.  Mazingira yabaki  safi ili kulinda viumbe hai,” ameeleza kiuongozi huyo ambaye pia ni mtaalamu wa mazingira.

Pia, Dk. Gwamaka amesema kwamba tarehe 5 Juni ni   siku ya mazingira duniani na kueleza kwamba siku hii imetengwa mahususi ili kuonyesha umuhimu wa mazingira.  Kwa kawaida nchini Tanzania  serikali  kwa kushirikiana na wadau wengine huitumia siku kutoa kauli mbiu muafana na hasa kwa kupanda miti.

“Mwaka huu hatukuadhimisha siku hiyo kutokana na janga la Corona. Lakini mwaka 2019  kauli mbiu ilikuwa ni: `Tumia mifuko mbadala wa Plastiki; kwa Ustawi wa Afya , Mazingira na Maendeleo ya Uchumi,” amesema Dkt. Gwamaka.

Dkt. Gwamaka amewahimiza Watanzania kuendelea kutiii sheria ya mazingira na kanuni zake.

 

 

 

 

 

 

Comments

Popular posts from this blog

Set aside land for investment, Kairuki tells RCs,district councils

Mkuu wa Mkoa Pwani asifu juhudi za mmiliki wa Makampuni ya Global Packaging na Wande Printing

17 projects to house 80,000 tonnes of crops being built