Kigoma yazindua mpango wa kupata mbolea ya bure toka Yara

 

Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Kamishna Thobias Andengenye(kulia) akimkabidhi mbolea  mmoja wa wakulima wadogo katika hafla ya  uzinduzi wa mpango wa kugawa mbolea bure kwa wakulima ujuliakanao kama "Action Africa"  unaoratibiwa na Kampuni ya   Mbolea ya Yara Tanzania.Kushoto ni Meneja biashara Kanda ya Magharibi   wa  YARA  Tanzania, Bw Phillipo Mwakipesile.

 

Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Kamishna Thobias Andengenye  wa pili kulia akimkabidhi mbolea  Mmoja wa wakulima wadogo katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa kugawa mbolea bure kwa wakulima ujuliakanao kama "Action Africa"  unaoratibiwa na Kampuni ya Mbolea ya YARA Tanzania. Kushoto ni Meneja Biashara Kanda ya Magharibi wa Yara  Tanzania, Bw Phillipo Mwakipesile na  Kulia ni  Mkuu wa  wa wilaya ya Kigoma Bw. Samson Anga.

 

Na Abdallah Luambano, Kigoma

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amezindua mpango wa kugawa mbolea bure kwa wakulima wadogo unaoratibiwa na Kampuni ya mbolea ya Yara Tanzania,  na kuwataka wakulima kutumia fursa hiyo kuongeza wingi wa punga na mahindi.

Akizungumza hayo kwenye hafla ya uzinduzi wa mpango huo unaojulikana kama ‘Action Africa’ na unaolenga kugawa tani elfu 12.5 za mbolea zinazokadiriwa kuwa na  thamani ya shilingi bilioni 16.5,  Bw Andengenya amesema kama mbolea hiyo itawafikia wakulima na wakaitumia vizuri, utakuwepo uhakiki wa kupata chakula na pato la wakulima kuongezeka.

“Ni mpango mzuri na unaopaswa kupongezwa na kila mpenda maendeleo ya wakulima wa nchi hii kwani utaongeza upatikanaji wa chakula na pia kipato cha mkulima mmoja mmoja hapa nchini na cha Taifa kwa ujumla,’’ amesema.

Aidha amewahimiza wakulima mkoani humo kujisajili ili waweze kunufaika na mpango  huo kwa kupiga simu *149*46*16#.

 RC Andengenye  ameziomba kampuni nyingine zinazosambaza zana na pembejeo za kilimo kuiga mfano wa Yara ili kuzidi kuimarisha sekta ya kilimo ambayo inaajiri Watanzania wanaokadriwa kuwa ni asilimia 65.

“Mpango huu pia utaongeza uhakika wa malighafi kwa viwanda vyetu vya ndani na serikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na Dk. John Pombe Magufuli,  inasimamia kwa bidii  ujenzi wa viwanda kote nchini,’’ amesema.

Meneja wa Biashara wa Yara,  Kanda ya Magharibi, Bw. Phillipo Mwakipesile, ameipongeza Wizara ya Kilimo kwa kuunga mkono jitihada za Yara hapa nchini.

‘’Shukurani zetu ziende kwa Wizara ya Kilimo kwa namna ambavyo imetuunga mkono kwa kipindi chote cha miaka 15 ya uhai wa Yara Tanzania.  Tunaamini  tutafanya makubwa zaidi siku za usoni  kwa manufaa ya wakulima na maendeleo ya Tanzania kwa ujumla,’’ ameeleza Bw. Mwakipesile.

Bw Semeni Gumwa ambaye ni mnufaika wa mpango huo  amesema kwa miaka mingi amekuwa hatumii mbolea na kuongeza kuwa anaamini  fursa ambayo imejitokeza  itamsaidia  kuongeza uzalishaji wa vipando vyake.

“Kwa miaka mingi hatujatumia mbolea katika uzalishaji wa mazao yetu.  Tunaamini mpango huu wa mbolea bure  utatusaidia kuongeza uzalishaji na kukuza kipato chetu,’’ amesema.

 

Comments

Popular posts from this blog

Set aside land for investment, Kairuki tells RCs,district councils

Mkuu wa Mkoa Pwani asifu juhudi za mmiliki wa Makampuni ya Global Packaging na Wande Printing

17 projects to house 80,000 tonnes of crops being built