Waziri Sima: NEMC haitakuwa kikwazo kwa wawekezaji
NAIBU Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Bw. Mussa Sima akizungumza na
waandishi wa habari mkoani Mtwara hivi karibuni jinsi Baraza la Taifa la Hifadhi
na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ambalo lipo chini ya Ofisi yake kwa namna
linavyopambana kuweka mazingira rafiki ili kuendelea kuwavutia wawekezaji hapa
nchini.
|
Waziri Sima: NEMC haitakuwa kikwazo kwa wawekezaji
Na Mwandishi Wetu, Lindi
Na Mwandishi Wetu, Lindi
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Bw. Mussa Sima amelipongeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi
wa Mazingira (NEMC) ambalo lipo chini ya Ofisi yake kwa namna linavyopambana
kuweka mazingira rafiki ili kuendelea kuwavutia wawekezaji hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ziara yake mkoani
Mtwara, Bw. Sima amesema kuwa licha ya changamoto zilizopo, ofisi yake imeendelea
kufanyia kazi mabadiliko mbalimbali ya kanuni na sheria ili kwenda sambasamba
na azma ya serikali ya ujenzi wa uchumi wa kati na viwanda pasipo kuathiri
mazingira.
“Tunapozungumzia mazingira tunazungumzia juu ya uhai wetu,
hivyo kama Wizara yenye jukumu la kusimamia mazingira tunalazimika kusimamia ustawi
wa jamii bila kuathiri uwekezaji,” alisema Bw. Sima
Bw. Sima amesema kuwa tayari ofisi yake imechukua hatua kadhaa ikiwemo kurekebisha baadhi ya tozo hali ambayo imepunguza malalamiko mengikutoka kwa wawekezaji.
Bw. Sima amesema kuwa tayari ofisi yake imechukua hatua kadhaa ikiwemo kurekebisha baadhi ya tozo hali ambayo imepunguza malalamiko mengikutoka kwa wawekezaji.
‘’Huko nyuma tulikuwa tukitoza asilimia moja ya jumla ya
mradi au biashara lakini sasa tumeganya miradi ambapo kila mradi utakuwa
na tozo yake. Mfano huko nyuma wamiliki wa visima vya mafuta walikuwa wanatozwa
mpaka milioni 10 lakini kwa marekebisho ya sasa watakuwa na
tozo ya milioni 4,’’ alisema Bw. Sima.
tozo ya milioni 4,’’ alisema Bw. Sima.
Sima aliongeza changamoto nyingine kuwa ni
uchelewashaji wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (EIA) ambapo ilikuwa
inachukuwa siku 149 lakini kwa marekebesho ya kanuni yaliyofanywa mwezi
Septemba, 2018 yalipunguza siku hizo na kuwa 95 tu.
“EIA ilikuwa inachukua muda mrefu sana na badaa ya
kutafakari kwa kina, tuliamua kufanya mabadiliko ya kanuni ambapo tumetoka siku
149 na sasa zimekuwa siku 95 hali ambayo inaonyesha ni kwa namna gani tumelenga
kurahisisha uwekezaji,’’ alifafanua Bw. Sima na kuongeza
“Tatizo la ucheleweshwaji wa EIA sio tatizo la NEMC bali ni
la Wataalamu Elekezi ambao wamekuwa na namna yao katika utekelezaji wa miradi,
hata hivyo tumeshakutana na tumeweka utaratibu wa tozo ambao unawiana na ule wa
serikali,”
Aidha alitumia nafasi hiyo kueleza mchango wa Wakaguzi wa
Mazingira ambao wapo kila mkoa kwa namna wanavyofanya kazi nzuri lakini
hawawezi kufanya nje ya utaratibu za mikoa.
“Natoa rai kwa wakaguzi wa mazingira kote nchini kutengeneza
mpango kazi na kuukabidhi ofisi ya mkoa ili watambulike wanafanya
kazi gani kwani hawa ni wadau muhimu sana katika mazingira na tuliwatumia
wakati wa utekelezaji wa katazo la ututumiaji wa mifuko ya plastiki,” alisema
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kupitia
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wameendelea
kuchukua hatua madhubuti katika kuhakikisha utekelezaji wa azma ya serikali ya uchumi
wa viwanda inatekelezeka pasipo kuathiri mazingira.
Comments
Post a Comment