Waziri Kairuki aitaka TPSF ishiriki kuboresha sheria za biashara na uwekezaji.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Mhe. Angellah kailuki.  (Kulia)  Akisalimiana na   Mwenyekiti wa taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Salum Shamte (kushoto)  Mara baada ya kuwasiri kwenye  Mkutano  Mkuu wa  19 wa Mwaka (AGM) wa Taasisi hiyo
uliofanyika  Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Mhe. Angellah kailuki.  (Kushoto) akizungumza  jambo na Mwenyekiti wa taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Salum Shamte ( kulia)  mara baada  ya kuwasiri kwenye  Mkutano  Mkuu wa  19 wa Mwaka (AGM) wa Taasisi
hiyo uliofanyika  Jijini Dar es Salaam. (Katikati) ni Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Bw. Godfrey Simbeye.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Mhe. Angellah kailuki.  (Kushoto) akizungumza  jambo na Mwenyekiti wa taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Salum Shamte ( kulia)  mara baada  ya kuwasiri kwenye  Mkutano  Mkuu wa  19 wa Mwaka (AGM) wa Taasisi
hiyo uliofanyika  Jijini Dar es Salaam. (Katikati) ni Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Bw. Godfrey Simbeye.

Waziri Kairuki aitaka TPSF ishiriki kuboresha sheria za biashara na uwekezaji.
Na Mosses Mahundi, Dar es salaam.

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Bi. Angellah Kairuki ameitaka Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi  Tanzania (TPSF) kushirikiana na ofisi yake  kupitia na kufanya marekebisho ya Sera ya Uwekezaji ya mwaka 1996 na Sheria ya Uwekezaji ya mwaka 1997 ili kuweka mazingira rafiki katika sekta nzima ya biashara na uwekezaji.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 19 wa taasisi hiyo mwishoni mwa wiki, Waziri Kairuki alisema kuna umuhimu mkubwa wa TPSF kushiriki katika zoezi hilo ili kutatua changamoto zinazohusu masuala ya uwekezaji wa ndani na nje ya nchi.

 “Ni mategemeo yangu nyinyi kama sekta binafsi mnaofanya shughuli mbalimbali za kibiashara mkigusa nyanja mbalimbali za maisha mtakua wazalendo kwa kuwekeza katika nchi yenu. mabadiliko hayo yataweka utaratibu utakaotoa kipaumbele kwa wawekezaji wa ndani ili kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha,” alisema Bi. Kairuki.


Alisema serikali inatambua  umuhimu wa ubia kati yake  na sekta binafsi  kwa kuipongeza pia  taasisi  kwa jukumu inalotekeleza  kama taasisi mwamvuli wa sekta binafsi nchini pamoja  na  kuwa mwenyekiti
wa kwanza wa Sekta Binafsi zote chini ya Baraza la Biashara la ukanda wa SADC kwa mwaka 2019/2020.


“Nitumie fursa hii kuipongeza tena taasisi kwa kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa serikali. Ni muhimu sana mkatambua kuwa katika uchumi wa kisasa wa karne ya 21 uimara wa taasisi za sekta binafsi ni nguzo muhimu sana,” alisema.

Waziri kairuki aliitaka TPSF  kutekeleza kwa vitendo kauli ya Mheshimiwa rais ya kuitaka taasisi kupanua wigo wa muundo wake kwa kufungua matawi vijijini, wilayani na mikoani ilikuwa na ushirikishaji
mkubwa

Rais Magufuli aliitoa Jijijni Dar  es Salaam  tarehe 7 Juni mwaka huu alipokutana na wawakilishi wa wafanyabiashara na wawekezaji. Pia alisisitiza ushiriki wa wanawake  na vijana kuchangamkia fursa hasa za kibiashara kama njia moja wapo ya kuunga mkono azma ya serikali ya awamu ya tano ya uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025.

“Hili ni jambo muhimu sana  na napenda kulisisitiza tena kwani itawasaidia kuimarisha  misingi ya taasisi yenu. Ni imani yangu kuwa mtaweza kuongeza ubunifu katika biashara na uwekezaji wenu,mtafanikiwa. Tujenge Tanzania , Tujenge Sekta Binafsi, kwa pamoja tujitegemee. Tunaweza.,” alisema.

Aidha Waziri Kairuki alisema serikali imetambua maeneo kutoka sekta binafsi na kuyaweka kama maeneo ya kipaumbele. Maeneo hayo ni pamoja na uanzishwaji wa viwanda nchini, kuendeleza  na kuimarisha miradi mikubwa ya kuendeleza miundo mbinu ya msingi na kutekeleza mabadiliko na maboresho ya sheria zinazolenga kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara na uwekezaji.


“Ninapenda kukumbusha  ushiriki katika utekelezaji wa miradi mikubwa mbalimbali  inayoendelea kutekelezwa hapa nchini kwa kufuata maelekezo na sheria ya manunuzi PPRA ili fursa zilizopo zisiwapite,” alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TPSF, Bw. Salum Shamte alisema mkutano huo ulikua wenye mafanikio makubwa na kuishuru serikali mchango mkubwa  ikiwemo kurudisha mrejesho juu ya mambo yaliyowasilishwa na mheshimiwa Rais Magufuli.

“Kama  taasisi tunafarijika kuona serikali ikituunga mkono kwa kushiriki nasi hasa katika kujadili changamoto zinazotukumba watanzania hasa katika sekta ya biashara na uwekezaji. Tumeshajadili
na wanachama na tumeridhia kuanza mchakato wa kurekebisha muundo wa taasisi hii ili kutanua wigo kwa watanzania waliopo mikoa mingine nje ya Dar es Salaam kujiunga na taasisi hii,” alisema.

Alimpongeza pia Waziri Kairuki kwa kazi nzuri na hatua mbalimbali anazozichukua kuakikisha sekta ya uwekezaji inapata msukumo stahiki na kutoa mchango mkubwa katika uchumi wa taifa kwa manufaa ya watu wote.

Naye  Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Bw. Godfrey Simbeye aliishukuru wizara ya uwekezaji  kwa kuipa  upendeleo  taasisi yake  kushiriki katika kurekebisha sera za uwekezaji katika biashara.

 “Serikali yetu inajali wananchi wake na ndiyo maana kila siku imekua ikitafuta namna ya kuhakikisha wananchi wake wanapata unafuu katika nyanja mbalimbali za maisha. Hivyo hatuna budi sisi kama taasisi kuhakikisha tunatoa ushirikiano wa hali na mali kwa wizara ya uwekezaji katika kutunga na kurekebisha sera na sheria za uwekezaji na baishara,” alisisitiza.

Comments

Popular posts from this blog

Set aside land for investment, Kairuki tells RCs,district councils

Mkuu wa Mkoa Pwani asifu juhudi za mmiliki wa Makampuni ya Global Packaging na Wande Printing

17 projects to house 80,000 tonnes of crops being built