Rais,Dkt.John Pombe Magufuli amepongeza Kampuni ya Unilever Tea Tanzania kwa kujenga kiwanda cha kisasa cha kuchakata majani ya chai Mkoani Njombe
Na Mwandishi wetu,Njombe.
Rais,Dkt.John Pombe Magufuli amepongeza Kampuni ya Unilever
Tea Tanzania kwa kujenga kiwanda cha kisasa cha kuchakata majani ya chai Mkoani
Njombe, nakuwataka watendaji Serikali kupunguza urasimu na vikwazo kwa
wawekezaji wanaotaka kuwekeza nchini jambo linalopelekea kuchelewa maendeleo.
Ameyasema hayo mkoani hapa alipokuwa katika uzinduzi wa
kiwanda cha chai cha Kabambe ikiwa ni
sehemu ya mwendelezo wa ziara yake katika mikoa ya Kusini na Nyanda za Juu
kusini mwa Tanzania na kuwataka watendaji wa Serikali kutowabugudhi wawekezaji
wenye nia ya kuwekeza nchini.
“Tumekuwa tukirudi nyuma kimaendeleo kutokana na urasimu wa
baadji ya watendaji Serikali hali inayopelekea kuchelewa kufikia malengo
tuliyojiwekea kama Serikali, hivyo niwatake watendaji wote kutekeleza majukumu
yao pasipo kuleta urasimu,” Alisema Rais Magufuli
Alisema mwekezaji atakayekwamishwa na mtendaji yoyote wa
Serikalini atoe taarifa katika ofisi yake ili hatua za kinidhamu zichukuliwe
dhidi ya huyo mtumishi ambaye anakuwa kikwazo cha uwekezaji nchini.
“Lazima watu wawajibishwe kwa vitendo vya urasimu
vinavyopelekea Nchi yetu kuonekana inavikwazo vingi katika uwekezaji, ijapokuwa
watu wachache ndio wanasababisha
mazingira hayo kwa sababu ya rushwa,”alisema Rais Magufuli
Aliongezea kuwa Serikali inapaswa kuandaa mpango kazi utakaotoa
mwongozo wa namna bora ya kulinda mazingira ya uwekezaji nchini na mikakati ya
kuvilinda viwanda vitakavyo jengwa kama cha Kabambe cha kuchakata chai.
“Zaidi ya Bilioni 49 zimewekezwa katika kiwanda hiki hivyo
ni lazima kuwe na mazingira bora ya kukilinda kiwanda hichi kwa hali yoyote ili
kiendelee kuotoa ajira kwa watanzania na kupeleke azma ya Serikali ya kujenga
viwanda kutekeleza kwa vitendo,” alisema Rais Magufuli
Aidha, Alipongeza Ubalozi wa Uingereza nchini, The Wood
Foundation, Kaibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Philemon Luhanjo, Spika wa Bunge
Mstaafu Mama Anna Makinda, Kituo cha Kuendelea Kilimo Nyanda za juu kusini mwa
Tanzania(SAGCOT) kwa kuwezesha kuwepo kwa kiwanda hicho mkoani Njombe.
“Niwatake wakulima wa chai mkoani Njombe kulima zao hili kwa
wingi kutokana na uwepo wa kiwanda cha kisasa cha kuchakata chai zaidi ya tani
elfu 150 ambapo asilimia 70 ya majani mabichi yanategemewa kutoka kwa wakulima
hali inayoibua fursa ya soko la majani mabichi, ,” alisema Rais Magufuli
Alisema kiwanda cha Kabambe kitapelekea kipato kwa mkulima
mdogo kuongezeka na kuchochea ukuaji wa uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla
kupitia kodi zitakazolipwa na kiwanda , hali itakayopelekea nchi kupiga hatua
kiuchumi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Unilever
Tanzania,Bwana David Minja alisema kampuni imetoa ajira zaidi ya watanzania
elfu 7 na kunufaisha watuzaidi ya elfu 40 kupitia kampuni za Unilever Tanzania
kikiwepo kiwanda cha kuchakata chai cha Kabambe.
“Tumejipanga katika kutoa mafunzo na elimu ya kilimo bora
cha chai ili wakulima waweze kulima chai yenye ubora utakao kubalika na
kupelekea soko la chai kuwa nzuri na kuwanufaisha wakulima kwa kupata vipato
vya juu,” alisema Bw.Minja
Alisema changamoto kubwa ni miundombinu ya barabara ya kutoa
chai mashambani na kufikisha kiwanda kwa wakati hali inayopelekea chai nyinig
kuharibika kabla ya kufika kiwanda kwa ajili ya kuchakatwa hivyo kumpelekea
mkulima hasara.
naye Balozi wa Uingeraza nchini Tanzania Bi.Sarah Cooke
alisema kufanikiwa kwa uwepo wa kiwanda cha kuchakata chai kutachochea
wawekezaji wengi zaidi kutoka Uingereza kuja kuwekeza Tanzania nah ii ni
kutoakana na uongozi mzuri wa Rais Dkt.John Magufuli katika kusimami sera ya
Viwanda.
“Maendeleo yanaletwa na viwanda hivyo kuwepo kwa viongozi
waadilif, mazingira bora na mikakati ya uwekezaji kutachochea wawekezaji wengi kuja kuwekeza
Tanzania, “ alisema Balozi Cooke
Mwisho.
Comments
Post a Comment