Tanesco: Azma ya uchumi wa kati na wa viwanda ifikapo 2025 inatekelezeka


     
Na jenny Chillery, Dar es Salaam
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema kuwa usambazaji wa umeme vijijini  unabadilisha maisha ya wananchi na umekuwa  ni chocheo kikubwa katika kutimiza azma ya serikali ya Rais John PombeMagufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchimi wa kati na wa viwanda ifikapo 2025.

Akizungumza katika mahojiano na katika kipindi kilichorushwa na Kituo kimoja cha Television Jijini Dar es Salaam,   Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dkt. Tito Mwinuka, amesema jana kuwa  Tanesco imekuwa ikishirikiana kwa karibu sana na Wakala wa Usambazaji Umeme Vijijini (REA) katika kupeleka umeme vijijini.  Ameshukuru REA kwa ushirikiano huo na kueleza kuwa ushirikiano huo umeongeza sana ujenzi wa viwanda vya kati, na kwamba  ujenzi wa viwanda umesaidia sana katika kubadili
maisha ya wananchi kiuchumi.

Kwa kuwa umeme umefika vijijini, ameeleza mtaalamu huyo, azima ya kufikia uchumi wa kati na wa viwanda ifikapo 2025 inatekelezeka. Amesema katika kipindi cha miaka minne iliyopita Tanesco imeunganisha zaidi ya vijiji 300 na umeme wa gridi.

“Tunawashukuru sana wenzetu wa REA kwa namna tunavyoshirikiana katika kusambaza umeme katika vijiji vya Tanzania. Kuwepo kwa umeme kukewafanya wawekezaji  wajenge viwanda vya kati na jambo hilo limeinua uchumi wa wananchi,” amesema kiongozi huyo.

Dk Mwinuka  ametaja  moja ya mafanikio makubwa ya Tanesco katika miaka minne ya iliyopita kuwa  ni kuiunganisha mikoa ya Njombe na Ruvumakwenye  gridi  ya taifa.

“Tanesco imejitihidi kuunganisha maeneo mengi na gridi ya taifa. Kuunganisha mikoa ya Njombe na Ruvuma na gridi ya taifa, kumeiwezesha serikali kuokoa zaidi ya shilingi bilioni 25, fedha ambayo imekuwa ikitumika kununulia mafuta mazito  ya kuendesha majenereta,” ameeleza.

Dk. Mwinuka ameishukuru serikali kwa kuiunga mkono Tanesco  katika kutekeleza mradi wa umeme wa Kinyerezi II, na kueleza kuwa mradi huo unachangia megawati  248 kwenye gridi ya taifa.

“Tanesco hatutakubali kuwa nyuma katika kuleta mageuzi ya kiuchumi hapa nchini. Tunataka kuona umeme unakuwa kiunganishi muhimu katika ujenzi wa viwanda na uchumi wa kati ifikapo 2025.  Tutajitahidi kuona wananchi wanapata umeme kwa gharama nafuu, hasa wanyonge, ili wafaidi matunda ya nchi yao.”

Mwisho.


Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa Pwani asifu juhudi za mmiliki wa Makampuni ya Global Packaging na Wande Printing

17 projects to house 80,000 tonnes of crops being built