Kilimo cha migomba, nanasi chazidi kupigiwa debe
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Kilimo cha migomba na mananasi kinatajwa kuwa na nafasi kubwa ya kumkomboa mkulima na kuchagiza maendeleo ya viwanda hapa nchini endapo kitapewa kipaumbele na wadau watashirikiana kwa karibu kukiendeleza.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya KilimOrgano, Bwana Ammar Mussaji, alipoongea na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam wanaofuailia uzalishaji wa miche ya migomba na nanasi kwa njia ya maabara (tissue culture) nchini Tanzania.
Mtaalamu huyo amesema mazao hayo yakilimwa kwa utaalamu na kuuzwa katika hali ya ubora wake yana bei nzuri na kwa hiyo yana tija kwa mkulima. “Kuna mahali pa kuanzia. Sisi tunawakaribisha wakulima na wenye viwanda ili tujadili namna ya kustawisha kilimo hiki kwa faida yetu wadau na nchi yetu.”
Tayari miche ya mazao haya imepandwa Tanzania Visiwani, Morogoro na Tanga na inaelezwa kwamba mazao yanayotokana na miche hii ni mazuri. Kadhalika Namibia, Uganda, Kenya na Ghana zinanunua miche hii na baadhi ya nchi za Marekani ya Kusini na Asia zinaagiza miche hiyo.
Juhudi inayofanywa sasa ni kueneza miche ya aina hii sehemu nyingi zaidi nchini, aneeleza mtaaalamu huyo.
“Kuna kila sababu ya kuhamasisha kilimo cha migomba na nanasi kwa njia za kisasa, kwani kina faida kubwa sana kwa wakulima na watengenezaji bidhaa kutokana na mazao haya. Tanzania ina nafasi nzuri sana ya kuzalisha kwa wingi mazao haya iwapo tutaingiza teknolojia ya kisasa na jambo hili linawezekana,” ameeleza mtaalamu huyo na kuongeza: “Mazao haya ni malighafi za viwanda ndani na nje ya nchi yetu. Aidha mazao haya ni chakula. Ndizi ni moja ya mazao yenye virutubisho vingi kwa afya ya wafanyakazi.”
Aidha Bwana Mussaji amesema kuwa kilimo cha migomba na nanasi kina nafasi kubwa hasa katika kipindi hiki ambapo Serikali ya Awamu ya Tano
inatekeleza sera ya viwanda na kufikia uchumi wa katika ifikapo 2025.
“Kilimo hiki kina nafasi kubwa katika kuimarisha viwanda nchini kwani mazao ya ndizi na nanasi ni malighafi muhimu kwa viwanda vya ndani na nje vinavyotengeneza vinywaji mbalimbali,” alisema na kuongeza “Tunawakaribisha watu wenye Viwanda ili waone namna gani wanaweza kutumia fursa za kupata malighafi za viwanda ambazo watatengeneza vinywaji lakini pia kwa matumizi ya chakula kwa kuwa ndizi ni moja ya nazao yenye virutubisho vingi kwa afya ya wafanyakazi.”
Kampuni hiyo yenye teknolojia ya kibayolojia ambayo huzalisha na kusambaza miche mbalimbali imetambuliwa kuwa ya Kimataifa na mashirika makubwa ikiwemo Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Taasisi ya Utafiti Tanzania (TARI) na Serikali ya Tanzania.
Bwana Mussaji amesema kilimo cha migomba na mananasi kina nafasi kubwa hasa katika kipindi hiki ambapo Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza Sera ya Viwanda na kufikia Uchumi wa Kati ifikapo 2025.
“Kilimo hiki kina nafasi kubwa katika kuimarisha viwanda nchini kwani mazao ya ndizi na mananasi hutumika kama malighafi viwandani ndani na nje ya nchi yetu. Ni mazao yanayotumika kutengeneza vinywaji mbalimbali,” alisema na kuongeza Kampuni hiyo yenye teknolojia ya kib aiolojia inafanya kazi kwa ukaribu na Wizara za Kilimo, Mifugo na Uvuvi Taasisi ya Utafiti Tanzania(TARI).
Mwisho.
Thanks for giving us good news. My I have your mobile number please Mr. Musaji?
ReplyDeleteKiting'ati S. M from Kisarawe district.