YARA yajizatiti kuchangia uimarishaji wa sekta ya kilimo
Na Abdallah Luambano, Dar es Salaam
Kampuni
ya YARA Tanzania imeahidi kushirikiana na serikali kwa karibu sana ili
kuhakikisha mpango wa ugawaji mbolea bure kwa wakulima nchini unakuwa wa
manufaa kwa wakulima na taifa kwa jumla.
Akizungumza
na waandishi wa habari juzi, siku chache baada ya uzinduzi wa ugawaji
wa mbolea uliofanyika Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni hiyo, Bw.Winstone Odhiambo, alisema mpango huo umelenga
kuhakikisha nchi za Afrika ikiwemo Tanzania zinajitosheleza katika
kuzalisha chakula. Kwa upande wa Tanzania mpango huo ni jitihada ya
kampuni yao kuchangia jihada ya serikali katika kuimarisha sekta ya
kilimo.
Lengo la kampuni
ni kuhakikisha uzalishaji wa mazao hususani mahindi na mpunga
unaongezeka katika nchi za Afrika kupitia mradi maalum wa kampuni
ujulikanao kama Action Africa,alisema Odhiambo
Alisema
mradi wa ugawaji mbolea bure ni moja ya miradi mikubwa ambayo
imetekelezwa tangu kampuni kuanzishwa nchini Tanzania miaka 15
iliyopita.
Naishukuru
Serikali ya Tanzania, kupitia Wizara ya Kilimo, kwa ushirikiano mkubwa
tulioupata ambao umetusaidia kuhakikisha azma ya kampuni yetu
inatekelezeka kwa vitendo na pia kwa kufanya tafiti za ubora wa mbolea
kupitia mamlaka za uthibiti zilizopo nchini , alisema Odhiambo
Aliongezea
kuwa ubora wa mbolea inayotolewa kwa wakulima umezingatia mazingira ya
ardhi ya Tanzania na kuongeza kwamba mbolea hiyo itatibu udongo na
kurutubisha aradhi na kwa hiyo mazao yatastawi vizuri na kuongezeka.
Mbolea
inayokwenda kwa wakulima ni NPK ambayo ni mahsusi kwa mazao ya mpunga
na mahindi, hivyo tani 12,500 zitagagiwa kulingana na vigezo na masharti
yaliyowekwa, alisema
Aidha,
Bw.Odhiambo alieleza utaratibu wa kujisajili ili kufanikiwa kupata
mbolea hizo ni kupitia namba *149*46*16# kwa mitandao yote ya simu,
hivyo wakulima waendelee kujisajili ili waweze kunufaika na mpango huu.
Pamoja
na kugawa mbolea kampuni itaendelea kutoa ushauri kwa wakulima juu ya
matumizi bora ya pembejeo na mbinu za kisasa za kidigitali za kuongeza
uzalishaji ili kuhakikisha nchi inazalisha chakula cha kutosha, alisema
Odhiambo
Alieleza kuwa
mpango huo mbali ya kuongeza chakula, ni sehemu pia ya kuunga mkono
juhudi za Serikali ya awamu ya tano nchi ya Rais Dkt.John Magufuli
katika kuendeleza kilimo ili kiweze kusaidia katika maono ya nchi ya
kufikia uchumi wa viwanda ifikapo 2025.
Comments
Post a Comment