Mshairi: Talanta ya mtu ni hazina ya ajira yake


Na Isdory Njavike, Dar es salaam

Mshairi chipuki, Aisha Kingu, jana Jijini Dar es Salaam amewaomba vijana wa Tanzania kuzienzi talanta zao na kuziendeleza kwani wakizitumia talanta hizo taratibu wataweza kujiajiri.

Akiongeza kwenye hafla ya uzinduzi wa kitabu chake cha mashairi ya Kiingereza kiitwacho Poetry Rebirth kijana huyo amesema talanta ya mtu imeficha fursa nyingi ikiwa ni pamoja na kujiajiri.   Ameeleza kuwa mafanikio ni matokeo ya kujituma, kazi ngumu  na yenye ustadi ndani yake na  ustahimilivu na kwamba talanta huibuka kutokana na kazi ya aina hiyo.

 Aisha Kingu  amesema kitabu hicho  kimebeba  mashairi 101 yanayogusa nyanja tofauti za maisha yakiwemo mashairi ya shukrani, upendo, mafanikio, na matumaini..

 “Nimeandaa hafla hii ili kupata nafasi ya kuwapa  hamasa  vijana wezangu wenye vipaji  kutambua na kuendeleza vipaji vyao ili viwe nyenzo muhimu katika kujiinua kiuchumi,”  amesema  Bi. Kingu.

Amewaomba wazazi kuwa mstari wa mbele katika kukuza na kuziendeleza talanta za  watoto  wao.   “Kama wazazi na walezi wataamua  kama kwa dhati watakuza  talanta   za vijana, basi sisi vijana  tutafika mbali sana kimaisha ,” amesisitiza Bi. Kingu.

Mzazi wa Aisha, Dk. Kingu Mtemi, amesema kuwa wao kama wazazi wametoa mchango wao ya kuendeleza kipaji cha mtoto wao licha ya kwamba binti huyo alikuwa akifanya vizuri sana katika masomo ya sayansi na walifikiri angekuwa daktari mzuri.

“Mwanzoni tulikuwa na wakati mgumu kwani tuliamini binti yetu angekuwa daktari lakini kadiri muda ulivyoenda tulizoea hali hiyo na kuamua kuunga mkono kipaji chake cha uandishi wa mashairi,” amesema Dk.Kingu.

Dkt Kingu amewasihi wazazi waendeleze  talanta za watoto Wao badala ya kuwalazimisha wafanye wayapendayo  wazazi au walezi.“Kupitia Aisha nimejifunza mengi. Natumia nafasi hii kuwasihi wazazi kuwa chachu ya kuendeleza vipaji vya watoto wao.”

Bw Musa Makange, mmoja wa waalikwa,  amegundua  nguvu ya kipaji cha mtu na jinsi kinavyoweza kumletea mafanikio makubwa kiuchumi na kutoa mchango chanya kwa jamii inayokuzunguka.

Bi. Aisha Kingu ameandika mashairi juu ya kazi za Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na kutokana na mashairi  ambayo ameandika siku za nyuma amekutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin na  Malikia wa Uingereza Elizabeth.

Comments

Popular posts from this blog

Set aside land for investment, Kairuki tells RCs,district councils

Mkuu wa Mkoa Pwani asifu juhudi za mmiliki wa Makampuni ya Global Packaging na Wande Printing

17 projects to house 80,000 tonnes of crops being built