Wajasiriamali wapongeza Mradi wa Viwanda Mbeya
Na Moses Mahundi, Mbeya
Wajasiriamali
wasindikaji wa mazao ya chakula mkoani Mbeya wakihojiwa Jijini hapa wamepongeza
hatua ya ujengaji viwanda vidogo Jijini hapa
katika mradi unaoratibiwa na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF).Mradi huo unasimamiwa Chama cha Wasindikaji Chakula na
Mazao(TAFOPA) na kufadhiliwa vikubwa na shika la Uswisi la HELVES.
HELVETAS
imekuwa na ikifadhili Mradi wa Kilimo Bora cha Mboga na Matunda kwa Wanawake na
Vijana(KIBOWAVI) na kwa ushirikiano na TPSF viwanda vidogo na mitambo ya baridi vinajengwa ili
kurahisisha usafirishaji wa mazao yanayokubalika masoko ya nchi za nje.
Bw
Renatus Lembileki amesema wakulima wanaongeza uzalishaji wa mazao kwa sababu
wanasababu ya kufanya hivyo. “Tuna matumaini makubwa sasa na tunaongeza
uzalishaji wa mazao. Tatizo kubwa
lilikuwa ni ardhi ya kujengwa viwanda, siyo fedha, au mazao au wakulima… bali
ardhi,” ameeleza mtaalamu wa kilimo mstaafu anayelima kabichi na maparachichi.
“Ni rahisi
kupata fedha au kwingineko kwa muda mfupi ili kuanzisha viwanda, lakini bila
ardhi utaviweka wapi? Hufiki kokote na hivi ndivyo imekuwa kwa muda
mrefu,”ameeleza mtaalamu huyo na kufafanua kwamba balaa la ugonjwa wa Corona
limeibua masoka mengi yenye kuhitaji bidhaa za kilimo kati nchi za mashariki,
kati, kusini mwa Afrika, Ulaya na Marekani. “Jamani watu huko wanahitaji mazao,
siyo maneno.”
Bw.Justin
Fungo wa Glosama Bakers amesema wajasiriamali wengi watapata sehemu za
kuzalisha bidhaa zao na kupata masoko ya uhakika.
“Mradi
huu utatuinua wengi kwani mtaji wa kununua mashine za kuchakata bidhaa umekuwa
ni tatizo kubwa. Pia mradi utakuwa chachu ya kuongezeka kwa uzalishaji wa
bidhaa na kupunguza upotevu wa mazao kwa kukosa soko,” ajmesema Bw.Fungo.
Ameipongeza serikali kwa kutoa ardhi ya
kujenga viwanda.
Bi
Syana Asalile wa Nuru Asili Farms amesifu mradi na kusema utapunguza uharibifu
wa mazao yao ya ufugaji na kilimo cha matunda kwani yatakuwa yanasindikwa jijini na kutafutiwa masoko ya
ndani na nje.
“Kwa
muda mrefu nimekuwa nachakata maziwa na natengeza juisi za matunda. Lakini bidhaa zetu zimekuwa zikiharibika.
Mradi huu utakuwa mkombozi kwangu,” amesema Bi.Asalile
Bw
Francko Jackson wa Jamii Kyela Products
ameupongeza ufadhili wa HELVETAS
na kusema utawafanya wajasiriamali wengi zaidi kujiajiri na kuongeza kwa
ubunifu katika kutengeneza bidhaa.
“Tatizo
la uharibifu wa bidhaa lilionekana kama vile halina utatuzi. Kukamilika kwa
mradi huu kutatufanya turasimishe bidhaa zetu kwenye mamlaka husika na kufanya
bidhaa zetu zikubalike katika masoko ya ndani na nje,” ameeleza.
Mwenyekiti
wa TPSF, Bi.Angelina Ngalula alipotakiwa kutoa maoni yake, amesema TPSF inafuatilia kwa karibu mradi huo na
kuongeza kwamba jitihada ya TPSF ni kutumia katika mikoa mingine uzoefu inaoupata
Mkoani Mbeya.
“Tunaendelea
kuhamasisha Mikoa mingine nchini kuandaa maeneo kwa ajaili ya ujenzi wa viwanda
hivi ili pale miradi itakapokuja iwe rahisi
kutekelezwa.”
Mwisho//
Comments
Post a Comment