TPSF yahamasisha vijana kulima mboga na matunda kibiashara
Na Moses Mahundi, Kilolo
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF) Bi.Angelina Ngalula, amesema jana hapa kwa kuwa mboga na matunda vina soko la uhakika ndani na nje ya Tanzania, vijana wakilima mazao haya watajiajiri haraka na kushinda umaskini kwa kiasi kikubwa.
Akiongea na wakulima wadogo baada ya kuvutiwa
na mashamba yao ya mboga na matunda katika Kijiji cha Mazombe. Wilaya ya
Kilolo, Mkoa wa Iringa na pia kusikiliza changamoto wanazowakabili, Mwenyekiti
huyo amewataka vijana wa Tanzania kulilma mboga na matunda na kutokana na adha
ya umasikini.
“Mboga na
matunda vina soko kubwa sana nje ya nchi hususani nchi za Ulaya. Jukumu letu
kuzalisha na kupeleka mzigo mingi nje ya
nchi na kuleta fedha ya kigeni nchini,” amesema Bi.Ngalula na kuwaomba vijana
wajiingize katika kilimo hicho.
Bi Ngalula
amesema moja ya changamoto kubwa nchini ni
kilimo chamazoea ambacho kinatoa
mazao yasiyokidhi ubora soko. “Tuna jukumu la kupeleka elimu ya kilimo
bora cha mboga na matunda kwa wakulima wetu kote nchini ili uzalishaji uwe na tija na mazao yaongezeke,”
amesema.
Amewapongeza
wakulima wa Mazombe na kuahidi kuwapeleka Mazombe wataalum kutoka Chama cha
Wakulima wa Mboga na Matunda Tanzania (TAHA) ili wawape ujuzi unaotakiwa na
kuinua kipato chao.
“Niwaomba vijana, hase wanawake, mjiunge katika vikundi
ili muweze kufikiwa kwa urahisi na watoa huduma mbali mbali, ikiwa ni pamoja na taasisi za kifedha
zinazoweza kuwapa mikopo,” amesema
Bi.Ngalula.
“Serikali inaendelea kutekeleza wajibu wake na kushirikiana na sekta binafsi. Hatua hizo ni pamoja na kuhakikisha biashara zinafanyika kwa urahisi na serikali inapata mapato yake na wafanyabiashara wananufaika na shughuli zao.”
“Serikali inaendelea kutekeleza wajibu wake na kushirikiana na sekta binafsi. Hatua hizo ni pamoja na kuhakikisha biashara zinafanyika kwa urahisi na serikali inapata mapato yake na wafanyabiashara wananufaika na shughuli zao.”
Mwenyekiti wa
kikundi hicho, Bw.Hassan Ally Kikoti, ameomba
TPSF iwaunganishe na taasisi za kifedha ili kukopeshwe na kuendelea kilimo chao.
“Changamoto
kubwa tuliyonayo ni mitaji ya kuendeleza kilimo cha mboga. Kwa kukosa fedha
tunazalisha kidogo kuliko mahitaji ya soko,” amesema Bw.Kikoti
Mmoja wa
wakulima, Bw Alex Msumile, amesema kilimo kweli kinatoa ajira lakini akaongeza
kwamba wanakabiliwa upatikanaji wa
masoko ya uhakika na bei nzuri kwa mazao yao. jambo ambalo limekuwa
likiwarudisha nyuma kimaendeleo.
“Niwaomba vijana
wenzangu tuelekeze nguvu kwenye kilimo.
Hii ni sekta yenye kumpa mtu
ajira na kipato,” amesema Bw Msumile.
Comments
Post a Comment