Christon boys wapongezwa matokeo mazuri kidato cha nne



Katibu tawala wa Wilaya ya Kisarawe, Bw.Mtela Mwampamba  katikati akizungumza  wakati wa Mahafali ya pili ya kidato cha Nne ya Shule ya Christon Boys  iliyopo kata ya  Msimbu Wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani iliyofanyika hivi karibuni.  kushoto ni  Afisa  Elimu vifaa na takwimu Bi. Alice Nkwera wa pili kushoto ni Mkuu wa Shule Bw. August Minja, kulia ni muwakilishi wa wazazi  Bw. Assah Mwambene  na wapili kulia ni  Mkurugenzi wa Shule ya Christon boys, Bi. Joyce Msuya.



Katibu tawala wa Wilaya ya Kisarawe, Bw.Mtela Mwampamba  (wapili kushoto) akisalimiana na muwakilishi wa wazazi  Bw. Assah Mwambene ( kulia) wakati wa Mahafali ya pili ya kidato cha Nne ya Shule ya Christon Boys  iliyopo kata ya  Msimbu Wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani iliyofanyika hivi karibuni. kushoto ni Mkuu wa Shule Bw. August Minja wapili kulia ni  Mkurugenzi wa Shule Bi. Joyce Msuya.


Na Isdory Njavike, Kisarawe

Serikali wilayani Kisarawe, Mkoa wa Pwani imeipongeza Shule ya Sekondari ya wavulana ya Christon  mkoani humo kwa kusimamia misingi
ya taaluma na kuiletea sifa kufuatia matokeo mazuri ya kidato cha nne 2019/2020.

Akizungumza katika Mahafali ya Pili ya Kidato cha Nne ya Shule ya hiyo ambayo kwa taratibu za shule hiyo hufanyika mara baada ya matokeo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe, Bw.Mtela Mwampamba mbali ya kuupongeza uongozi wa shule na kamati ya wazazi aliwataka wanafunzi kudumisha nidhamu na kuongeza zaidi juhudi ya kujisomea.

“Ufaulu huu ni mzuri na sisi kama serikali ya wilaya tumefurahishwa sana na matokeo yenu ya kidato cha nne. Tunawapongeza walimu, wanafunzi na wazazi kwa kushirikiana kuhakikisha wanafunzi wanasoma kwa bidii na kufaulu vizuri katika mitihani ya kitaifa,” alisema Bw.Mwampamba.

Alisema Sekondari ya Christon  imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani ya kitaifa kidato cha nne na cha pili na kuwa  mfano mzuri katika wilaya  ya Kisarawe  na hivyo kuzitaka shule nyingine kufuata nyayo.

Kwa mujibu  wa DAS  shule  hiyo mbali ya kuwa mfano  wa kuigwa kitaaluma kiwilaya pia imekuwa ikishirikiana  na serikali  katika nyanja mbalimbali  hata  wakati wa kukimbiza mwenge Mwaka jana waliweza  kugharamikia chakula  na kuifanya wilaya hiyo  kuwa ya
kwanza kimapokezi  kwa mkoa wa Pwani.

‘’Nipende kuwapongeza sana Christon kwa namna ambavyo mmefanya vizuri katika Mtihani wa Taifa na kushika nafasi ya kwanza katika Wilaya yetu lakini pia namna inavyojitoa kushirikiana na Serikali  katika Nyanja mbalimbali,’’ alisema Bw. Mwampamba.

Mbali ya hiyo alisema Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli imefanikiwa   kuiunganisha wilaya hiyo kwenye umeme wa  gridi ya taifa ambapo mwananchi inatugharimu shilingi 27,000 kuunganishwa kwa huduma hiyo.

‘’Wilaya yetu ya kisarawe inajumla ya vijiji 84, mpaka sasa  vijiji 72 vimeshaunganishwa na umeme wa gridi ya taifa, vimebaki vijiji 12, ambapo usimamishwaji wa  nguzo  za umeme umeshaanza,’’ alisema Bw.Mwampamba.

 Awali Mkuu wa Shule Bw. August Minja aliipongeza Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri wanayofanya katika kuhakikisha kuwa lengo la  kujenga uchumi wa kati na  viwanda ifikapo mwaka 2025 unatimia.

“Sisi kama Christon boys tumeshaanza kutekesa  azma ya serikali kwa vitendo kwa kuwaandaa  wanafunzi  kwa ajili ya kujitegemea  wawe na elimu ya ziada  ukiachilia mbali ile ya darasani ambayo itatoamchango chanya  kwa serikali pamoja na jamii kiujumla,’’ alisema Bw. Minja.
Bw.Minja aliwashukuru wazazi na walezi kwa kuwaamini  kuwapa  watoto ili wapikwe kitaalama na maadili ya kitanzania na kuahidi kuendelea kjutoa elimu bora na inayokidhi matarajio ya taifa.

“Tunaishuru serikali serikali ya Wilaya ya Kisarawe kwa kutupatia ushirikiano mkubwa wakati wote tunapohitaji. Ushirikiano wetu namajirani pamoja na shule mbalimbali wilayani hapa na mkoa kwa ujumla ni mzuri na tunajivunia,” alisema Bw. Minja.

Naye mwakilishi wa  wazazi ,Bw. Assah Mwambene  aliupongeza uongozi wa shule hiyo kwa juhudi wanazochukua  kuhakikisha wanawajenga wanafunzi kitaaluma, kimalezi sambamba na maadili ya kiroho.

‘’ Mahali panapostahili sifa ni vizuri tukasema, kiukweli sisi kama wazazi tunashukuru uongozi mzima wa shule kwa  juhudi zenu mnazochuku katika kuhakikisha mnatoa elimu bora na siyo bora elimu,’’ alisema Bw.Mwambene.


Comments

Popular posts from this blog

Tanzania praised for being keen on fertilisers going to farmers

NEMC warns on emptying effluent in built-up areas, flood waters

Mbeya agro-processors get 5 acres to build 50 industries