Majaliwa asifu wajenzi wa kiwanda cha sukari Bagamoyo
Na Abdallah Luambano, Bagamoyo
Waziri Mkuuu Kassim Majaliwa amesifu wajenzi wa Kiwanda
cha Bagamoyo (BSL) kinachofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo
(TADB) kwa shilingi bilioni 15 na kusema kukamilika kwa kiwanda hicho
kutapungaza uagizaji wa sukari kutoka nje.
Akizungumza na wageni na wafanyakazi wa kiwanda hicho jana, Waziri Mkuu amesifu ujenzi wa kiwanda hicho na kusema:
“Mahitaji
ya sukari ya mezani kwa sasa hapa nchini ni tani 450,000 , uzalishaji
wetu ni tani 380,000. Tuna upungufu wa tani 70,000. Niwapongeze
wawekezaji wanaojenga kiwanda hiki na taasisi zote za fedha kwa
jitihada zilizochukuliwa mpaka kujengwa kwa kiwanda hiki. Kiwanda
kikianza kufanyakazi tutaweza kukidhi mahitaji ya yetu ya ndani,’’
amesema Waziri Mkuu.
Waziri
Mkuu amewataka Watanzania kubadilika na kuanza kujivunia bidhaa
zinazozalishwa nchini na kutokana na kasumba ya kuamini bidhaa za nje
ni nzuri zaidi.
“Rais
wetu Dk. John Pombe Magufuli huwa anasema tunaweza na leo nimethibitisha
pasipo na mashaka yoyote kwamba Watanzania tunao uwezo wa kifedha
kufanya uwekezaji, wataalamu wa kuendesha mitambo na hata usimamiaji wa
miradi mikubwa, tujivunie hilo,’’ amesema.
Mkurugenzi
wa Makampuni ya Bakhresa, Bw. Abubakar Bakhresa, mbali ya kumshukuru
Rais Magufuli kwa kuwapatia shamba lenye hekta 10,000, ambalo
watalitumia kuzalisha miwa na ameahidi kuendelea kuunga mkono jitihada
za serikali za kuipeleka nchi kwenye uchumi wa viwanda.
“Tunamshuru
Rais Magufuli kwa kutupatia eneo hili ambalo tutalitumia kuzalishamiwa
kama malighafi ya kiwanda. Jambo muhimu zaidi kwetu ni kuendelea kuunga
juhudi za serikali za kujenga uchumi wa viwanda ifikapo 2025,’’
amesema.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine, amesema mbali ya kuwezesha
kiwanda hicho, Benki imelenga pia kuwanufaisha wakulima wadogo wa miwa.
“Kwa
kawaida wenye mabenki hawawezi kumkopesha mkulima bila kuliona eneo.
Sisi tumeona fursa. Fursa hiyo ni kwamba awamu ya pili ni kuhakikisha
uzalishaji unakuwa endelevu. Katika fursa hii na awamu hii
tutawakopesha wakulima wadogo kwa masharti nafuu ili waendeleze mashamba
yao,’’ amehadi Bw. Justine.
Mkurugenzi
wa Mahusiano wa Makampuni ya Bakhresa, Bw. Hussein Sufian, amesema
gharama za mradi ni Dola za Marekani milioni 100 ambapo TADB imetoa Dola
za Marekani milioni 6.5 sawa na shilingi za bilioni 15.
Mabenki
mengine ni CRDB Bank ambayo imetoa dola milioni 25, Standard Chartered
imetoa dola milioni 10 na dola milioni 30 zimetolewa na makampuni ya
Bakhresa na kufikisha asilimia 70 ya mtaji wa mradi wa ujenzi wa
kiwanda.
Comments
Post a Comment