Dampo la Nsalaga Uyole hatari kwa afya za watu na mazingira, aonya Suma
-->
-->
-->
![]() |
NAIBU
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Bw. Mussa Sima wa pili
kushoto akipewa maelezo na Mkuu wa hifadhi ya Taifa ya Ruaha
Bw Izumbe Msindai (SACC) Wakati alipotembelea eneo Mfereji wa
umwagiliaji wa mnazi, uliopo wilayani mbalali unaopakana na
Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambao utumika katika skimu za kilimo cha zao la
Mpunga. Wakati wa ziara yake ya kikazi kukagua uzingatiaji wa
Sheria ya Mazingira katika mikoa ya nyanda za juu kusini. Wa pili
Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira nchini (NEMC),Prof. Esnati Chaggu, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa
NEMC, Dkt. Samuel Gwamaka, Na wa tatu kulia ni ni Mkuu wa
Wilaya ya Mbalali Bw. Reuben Mfune.
![]() |
NAIBU
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Bw. Mussa Sima
kushoto akipewa maelezo na Mkuu wa hifadhi ya Taifa ya Ruaha
Bw Izumbe Msindai (SACC) wa pili kushoto Wakati alipotembelea
eneo Mfereji wa umwagiliaji wa mnazi, uliopo wilayani mbalali
unaopakana na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambao utumika katika skimu za
kilimo cha zao la Mpunga. Wakati wa ziara yake ya kikazi kukagua
uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika mikoa ya nyanda za juu
kusini. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Hifadhi na
Usimamizi wa Mazingira nchini (NEMC),Prof. Esnati Chaggu, Wa pili kulia
ni Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Samuel Gwamaka, Na wa tatu kulia
ni ni Mkuu wa Wilaya ya Mbalali Bw. Reuben Mfune.
Na Isdory Njavike, Uyole
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Bw.
Mussa Sima, ameghadhabishwa na ujenzi duni wa dampo la taka la Nsalaga
Uyole, Mkoani Mbeya, na kuonya kwamba miundombinu hni hatari kwa afya za watu
na mazingira kwa ujumla.
Amelitaka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini
(NEMC) kushirikiana na ofisi za Mkoa wa Mbeya ili kupata ufumbuzi wa tatizo
hilo kwani dampo limejengwa bila kuzingatia kanuni za kuhifadhi mazingira na
pia utupaji taka kwenye dampo umekuwa ukirudidha uchafu kwenye makazi ya
watu. Taarifa alizopata ni kwamba dampo limejengwa bila utafiti wa
kitaalamu wa kutosha.
Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo la Nsalaga Uyole,
katika ziara yake ya kikazi kukagua uzingatiaji wa
Sheria ya Mazingira. katika mikoa ya nyanda za juu kusini, amekumbusha kwamba
taka lazima zitenganishwe kwenye vyanzo kabla ya kuingizwa kwenye dampo.
“Kuanzia sasa watafutaji taka wasiruhusiwe kuingia kwenye mashimo ya
dampo kwani wamekuwa wakirudisha uchafu kwenye makazi ya watu na kuchafua
mazingira,” amesema naibu waziri huyo.
Bw. Sima ambaye ameambatana na na Mwenyekiti wa Bodi
ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini (NEMC),Profesa
Esnati Chaggu, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk. Samuel Gwamaka pamoja na
maafisa wengine wa NEMC, amewataka wasimamizi wa dampo hilo kujifunza
kutoka kwa wasimamizi wa madampo katika mikoa mingine ambako madampo ya
kisasa tayari yamejengwa na yanahifadhi mazingira.
“Halmashauri ya Mkoa wa Mbeya mjipange na kuhakikisha mnatenga
eneo maalum ya shughuli za urejelezaji ili kuondoa mlundikano wa
uchafu, kwani mmekuwa mkichanganya uchafu na taka ngumu ambazo ni ngumu
kuzizoa,” ameagiza naibu waziri huyo.
Prof. Chaggu amesema majitaka yatokayo katika dampo (leach ate)
yana sumu kiasi kikubwa na kufafanua kwamba majitaka hayo yana asilimia 8 juu
ya majitaka yatokayo majumbani. Ametaka majitaka hayo yasimamiwe kwa umakini
ili yasitiririke katika mazingira na kudhuru jamii inayoishi karibu na dampo
hasa katika kipindi cha mvua.
Prof. Chaggu amesema utunzaji wa mazingira unapozingatiwa,
mazingira yanakuwa salama na afya za Watanzania zinaboreka na uchumi unakua.
Dk Gwamaka amefafanua kwamba kwa mujibu was Sheria ya Mazingira na
Kanuni za Usimamizi wa Taka ngumu, halmashauri za wilaya zina wajibu wa
kutenganisha taka na kuelimisha wananchi jinsi ya kufanya hivyo.
“Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004, kuna Kanuni za Usimamizi
wa Taka ngumu ambazo zimeeleza kwa mapana wajibu wa halmashauri za wilaya
juu ya kutenganisha taka na kuelimisha wananchi jinsi ya kufanya hivyo. Wakati
ni huu wa kutekeleza maagizo hayo kwa kuanza kutoa elimu. Tutashirikiana
kwa karibu na halmashauri kuhakikisha tunalitimiza hilo”. ameahidi Dk. Gwamaka.
Amefafanua kuwa taka ni fursa na kutoa mifano kwamba taka za
glasi na plastiki zinaaweza kuwa malighafi kwenye viwanda vya urejelezaji
na kukuza uchumi kwani viwanda vinalipa kodi kwa serikali.



Comments
Post a Comment