NEMC kuchagiza kasi ujenzi wa viwanda nchini
Na Abdallah Luambano, Dar es Salaam
BARAZA la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),limejipanga kufanikisha azma ya Serikali ya Awamu ya Tano chini Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kujenga uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Samuel Gwamaka alisema nafasi ya baraza ni kubwa katika kufanikisha ujenzi wa viwanda kama taasisi mtambuka inayochagiza maendeleo na ukuaji wa sekta mbalimbali za uchumi.
“Tumekuwa tukishirikiana kwa karibu sana taasisi nyingine za serikali kama Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) na nyinginezo katika kufanikisha azma ya serikali ya kujenga uchumi wa
kati na viwanda,” alisema Dkt. Gwamaka.
Alisema baraza halitakuwa kikwazo katika kufanikisha ujenzi wa viwanda zaidi ya kuwa mshauri kwa wawekezaji wa viwanda kuzingatia sheria na taratibu za kimazingira bila ya kuathiri afya za wananchi.
“Sisi kama baraza tunapenda kumshauri mwekezaji kiwanda tangu anapoanza ujenzi au uzalishaji nini anapaswa kuzingatia ili uwekezaji wake uwe rafiki wa mazingira,” alisema na kuongeza kuwa NEMC inaunga mkono azma ya ujenzi wa viwanda.
Dkt. Gwamaka alisema milango ipo wazi ofisi zote za NEMC makao makuu na zile kanda kwa mtu yeyote anayejenga kiwanda kwenda kupata ushauri kwani baraza limekamilika na lina waatalamu katika sekta mbalimbali.
“Tunaweza kuangalia kumshauri mwekezaji wa kiwanda kuwa eneo gani anaweza kuboresha. NEMC ni kampuni wezeshi kwa mtu au mwekezaji yeyote anayefuata na kuheshimu sheria za mazingira,” alisema.
Dkt. Gwamaka alisema uchumi wa nchi yeyote duniani hauwezi kuwa imara na endelevu bila kuwa na viwanda kwani sekta ya viwanda ndiyo ya muhimili au roho ya uchumi.
Bosi huyo wa NEMC hakusita kupongeza hatua na juhudi za makusudi zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano kwa kusema viwanda vitapanua na kuongeza wigo wa ajira kwa vijana wa kitanzania.
“NEMC ni mdau mkubwa katika ujenzi wa viwanda. Tunahamasisha viwanda vinavyoleta tija,rafiki kwa mazingira na kulinda afya za wananchi,” alisema Dkt. Gwamaka.
Serikali ya awamu ya tano tangu iingie madarakani miaka mitatu iliyopita imeweka hadharani dhamira yake ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025 na tayari hatua mbalimbali zimeshachukuliwa kufanikisha azma hiyo.
Mwisho.

Comments
Post a Comment