Wafanyakazi wa Tanesco wenye nguzo za umeme wapokelewa kwa shangwe Christon Boys


 Na Mwandishi wetu, Kisarawe

KATIKA kipindi kisichozidi miezi mitatu tangu Naibu Waziri wa Nishati,  Bi. Subira Mgalu, alipoitembelea Shule ya Sekondari ya Wavulana ya
Christon na kuagiza Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuiunganisha shule hiyo na gridi ya taifa, jana nguzo za umeme zimedondoshwa katika eneo lililopimwa kwa ajili hiyo.

Upelekaji wa nguzo hizo jana umeibua shangwe na furaha kutoka kwa wanafunzi, wafanyakazi na wakazi wa eneo linalozunguka shule hiyo.
Ofisa wa Tanesco, ambaye hakutaja jina lake, amesema kuwa kutokana na mchango wa shule hiyo katika kuinua taaluma Mkoani Pwani, shirika limeona  ni wakati mzuri kutekeleza agizo la naibu waziri.

“Itakumbukwa kwamba wakati Naibu Waziri alipotembelea shuleni hii alitoa maagizo ya kuiunganisha  na gridi ya taifa. Tumeleta nguzo hizi
ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo hayo na muda sio mrefu tutaanza zoezi la kuunganisha nyaya kwa wateja wetu,” amesema ofisa huyo.

Shule hiyo imekuwa ikitumia gharama kubwa katika kununua mafuta ya kuendesha majenereta na kukosa umeme wa uhakika kwa sababu
haikuunganishwa na gridi ya taifa.

“Moja ya kero ambayo Naibu Waziri alielezwa na uongozi wa shule wakati alipofanya ziara shuleni hapo ni kukosekana kwa umeme wa uhakika.
Tanesco tumesikia na muda sio mrefu wataiunganisha na gridi ya taifa,” ameahidi ofisa huyo wa Tanesco.

 Mkuu wa Shule, Bw. August Minja hakuwepo  kuzungumzia tukio  hilo zuri . Mkazi wa eneo hilo, Bw Idd Shabani,  amefurahishwa na tukio hilo na
kueleza kuwa katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli,  familia maskini na tajiri zinafursa sawa ya kupata umeme.

“Tunamshukuru Naibu Waziri kwa agizo la kuunganisha shule ya Christon na gridi ya taifa. Umeme hautasaidia shule tu bali hata sisi wakazi wa
eneo la  karibu na shule hii. Kupata  umeme ilikuwa ni ndoto isiyotekelezeka kwa siku za nyuma,” amesema Bw. Shabani.

Bw. Shabani amesema pia kuwa kuwepo kwa umeme katika eneo hilo kutawavutia wawekezaji wa kujenga viwanda vya kuchakata mazao ya
kilimo, kuibua na kukuza shughuli za kibiashara.Shule ya Sekondari ya Wavualana ya Christon imekuwa na rekodi nzuri ya kitaaluma kitaifa na ni kati ya shule bora katika Wilaya ya Kisarawe

.
Kwa muda mrefu shule hiyo imekuwa ikikabiliwa na ukosefu wa umeme wa uhakika.  Tatizo la umemme limekuwa likizua changamoto mbali mbali
katika kutekeleza shughuli za kitaaluma na miradi ya shule ya kujitegemea.

Comments

Popular posts from this blog

Set aside land for investment, Kairuki tells RCs,district councils

NEMC warns on emptying effluent in built-up areas, flood waters