Maabara ya kisasa ya kupima afya ya udongo kwa kutumia gari maalum yazinduliwa

Maabara ya kisasa ya kupima afya ya udongo kwa kutumia gari maalum yazinduliwa
Na Mwandsihi Wetu, Arusha
TEKNOLOJIA ya maabara ya kupima afya ya udongo kwa kutumia gari
maalumu lenye uwezo kupima zaidi ya sampuli 100 za udongo kwa siku
moja limezinduliwa hapa nchini ili kupima udongo na kumhakikishia
mkulima  uzalishaji wa mazao kwa wingi na yenye tija sokoni.
Uzinduzi wa Teknolojia hiyo kutoka nchini Uholanzi ulifanyika jijini
Arusha kati ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania Bw.Abdallah
Ulega kwa niaba ya Tanzania na Makamu Waziri wa Kilimo na Ubora wa
Chakula wa Uholanzi, Bi.Marjolijn Sonnema kwa niaba ya nchi yake ili
kufanikisha mageuzi katika sekta ya kilimo.
Akizungumza mara baada ya kufanya uzinduzi wa teknolojia hiyo, Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Bw Ulega aliishukuru Serikali ya Uholanzi
kwa kutoa teknolojia yake kwa Tanzania na kusema kuwa itasaidia kuleta
mapinduzi katika uzalishaji mazao.
“Kupima afya ya udongo inatoa majibu juu ya ubora wa ardhi husika,
mazao yanayofaa kulimwa katika eneo hilo, kiwango cha mbolea
kinachotakiwa na kutoa makadirio ya kiwango cha mavuno katika eneo
husika,” alisema Naibu Waziri Ulega
Aliongezea kuwa gharama ya kupima shamba iliyowekwa ya shilingi 25,000
mpaka 30,000 wakulima wanaweza kumudu na kuwataka wapema mashamba yao
kabla ya kufanya kilimo ili kujua matatizo yaliyopo kwenye ardhi yake
na nini afanye ili tija ya uzalishaji iongezeke.
“Teknolojia hii imeletwa kwetu hivyo tunakila sababu ya kuhamasisha
wakulima nchini kupima mashamba yao ili wajipatie uhakika wa zao
lilalofaa katika ardhi yake na nini afanye katika kuboresha ili aweze
kuongeza tija ya uzalishaji,” alisema
Naibu Waziri Ulega aliesema kuwa mageuzi katika sekta ya kilimo
yatapatikana kupitia teknolojia hii ya kupima afya ya udongo na
kupelekea kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo hali
itakayochochea ujenzi wa viwanda vya kuchakata na kuongezea thamani ya
mazao.
“Ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi kunachochea kasi ya
maendeleo kwa kuibua teknolojia na ujuzi mbalimbali katika kuiletea
nchi maendeleo, naipongeza kampuni ya Life Support System Tanzania
(LSSL)  kwa kuwekeza kwenye ketnolojia hii,” alisema Ulega
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa LSSL, Dkt.Edmond Matafu alisema
magari manne yapo tayari pamoja na handheld soil scanner 100 ambazo
zitatumiwa na maafisa ugani kwa ajili ya kuchukua sampuli za udongo
katika maeneo ya vijiji kote nchini.
“Hii itasaidia kufanya zoezi la kupima afya ya udongo kwa wakati
pasipo kuchelewa kipindi cha kulima ambapo itampa unafuu mkulima kujua
mahitaji katika shamba lake ili aweze kupata tija katika uzalishaji
mazao,” alisema Dkt.Matafu
Aliongezea kuwa juhudi za Serikali za kujenga uchumi wa kati na
viwanda zitatekelezeka kwa ushirikiano kati ya sekta binafsi na
Serikali kufanya kazi kwa pamoja kuhakikisha vikwazo vyote
vinavyokwamisha maendeleo vinatatuliwa ili maendeleo tunayoyatarajia
yaweze kufikiwa kwa vitendo.
“Zoezi la kupima afya ya udongo litafanyika kote nchini kwani
tumejipanga vizuri katika kutoa huduma hii kwa wakulima hivyo
ushirikiano ndio kitu muhimu katika kufanikisha zoezi hili ambalo
litakwenda kuinua hali ya uzalishaji zao nchini,” alisema Dkt.Matafu
Uzinduzi wa Maabara ya kupima udongo kwa kutumia gari maalum
ulishuhudiwa na Makamu Waziri wa Kilimo na Ubora wa Chakula kutoka
Uholanzi, Bi. Marjolijn Sonnema, Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania
Joroen Verheul, Katibu Mkuu Wizara ya Mifungo na Uvuvi Profesa
Elisante Ole Gabriel na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew
Mtigumwe na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kuendeleza Kilimo Nyanda
za Juu Kusini, Bw. Geoffrey Kirenga..
Mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

Mbeya agro-processors get 5 acres to build 50 industries

Tanzania praised for being keen on fertilisers going to farmers

Majaliwa aitaka YARA kuongeza uwekezaji katika sekta ya kilimo..