NEMC yashauri sheria ya mipango miji ifuaate ili kulinda Mazingira



Na Isdory Njavike, Mwanza
BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamzi wa Mazingira(NEMC) limetoa wito kwa wafanyabiashara na wawekezaji hapa nchini kufuata sheria na taratibu za mipango miji ili kuepuka ujenzi holela wa viwanda katika makazi ya watu  na kusababisha kero kwa wananchi.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Mwanza katika ziara ya kukagua uzalishaji wa mifuko mbadala na kubaini iliyochini ya kiwango, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt.Samuel Gwamaka alisema sheria zikizingatiwa katika ujenzi wa viwanda na shughuli nyingine itasaidia kulinda mazingira.
“Ujenzi wa viwanda katika makazi ya watu unasababisha kero kwa wananchi kutokana na kelele, harufu au vumbi, ili kuepukana na hilo ni lazima wawekezaji kwenye viwanda wakafuata taratibu za mipango miji ili kuepusha adha kwa wananchi,” alisema Dkt.Gwamaka.
Alisema ujenzi unaofuata utaratibu wa mipango miji unasaidia kuyafanya mazingira kuwa salama na kupelekea huduma nyingine kufanyika kwa urahisi kama vile kuainisha idadi ya viwanda na mahali vilipo inakuwa rahisi tofauti na hali ilivyo kwa baadhi ya maeneo nchini.

“Ushirikiano kati ya taasisi za serikali na wafanyabiashara, wajasiriamali na wawekezaji unahitajika ili  hatua anayofanya mwekezaji katika uwekezaji wake iendane na taratibu za Serikali  hali itakayosaidia kukuza uwekezaji wa viwanda unaofata utaratibu nchini,” alisema Dkt.Gwamaka

Alisema shughuli zote za uendelezaji wa makazi na upangaji wa mautumizi ya ardhi zinasimamiwa na halmashauri za wilaya, miji, manispaa na majiji kwa niaba ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi hivyo NEMC tunashirikiana nao katika kuhakikisha mazingira yanatunza kupitia mwongozo wa mipango miji.

 “Jukumu letu kubwa ni kuhakikisha shughuli za binadamu nchini hazileti athari katika mazingira ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini ya athari kwa mazingira kutokana na shughuli husika hali inayosaidia mazingira kuwa salama kwa kizazi cha sasa na baadae,” alisema

Aidha, Dkt.Gwamaka aliwataka wajasiriamali waliojenga viwanda vyao katika makazi ya watu kuwasiliana na mamlaka husika ili waweze kupatiwa mwongozo wa kuhamisha viwanda hivyo kwend akwenye maeneo maalum ya viwanda ili kuepusha uchafu wa mazingira katika makazi ya watu.

“Mipango madhubuti ya ujenzi wa miundombinu, ulinzi wa mazingira ya asili, kuboresha mazingira ya kuishi na utunzaji wa mazingira hufanya mji  ukue kwa urahisi na kwa ufanisi pasipo kuathiri mazingira hali itakayopelekea kuzidisha thamani ya ardhi na kuvutia wawekezaji zaidi,” alisema Dkt. Gwamaka

Aliongezea kuwa NEMC itaendelea kushirikana na wadau wote ili kuhakikisha sheria na mwongozo wa mipango miji inatekelezeka kwa wawekezaji kujenga viwanda katika maeneo yanastahili kuwekwa viwanda ili kufanya miji kuwa katika hali ya usalama kimazingira. Kwa upande wake Mmiliki wa kiwanda cha Chilya’s Tubing kilichopo Mwanza mjini, Bw.Spenas Masatu alisema ushauri wa NEMC ameupokea na ataufanyia kazi kwanza kwa kuhamisha kiwanda chake kukipeleka katika
maeneo ya viwanda.
“Nipo kuunga mkono azma ya Serikali ya kujenga viwanda hivyo taratibu zote ni lazima nizifuate ikiwa ni pamoja na kukiweka kiwanda change katika eneo linalotakiwa,” alisema Bw.Masatu
 Ziara ya ukaguzi wa viwanda vya kuzalishaji mifuko mbadala nchini na inayoingizwa kutoka nje ya nchi imeanzishwa kutoka na kuongezeka kwa mifuko iliyochini ya kiwango cha gsm 70 na kutokuwa na lebo na anwani ya mzalishaji hali iliyopelekea biashara kwa wazalishaji wanaofata viwango na kanuni kukosa soko la bidhaa zao.

Mwisho.


Comments

Popular posts from this blog

Tanzania praised for being keen on fertilisers going to farmers

Gold mine in Songwe wins ministerial praise for protecting environment

NEMC warns on emptying effluent in built-up areas, flood waters