Buchafwe ahimizwa kusoma vitabu kuongeza maarifa
Watanzania, hususani vijana,
wametakiwa kujenga utamaduni wa kusoma vitabu ili waweze kupata na kuongeza maarifa ili waweze kufikia ndoto
zao katika maisha.
Wito huo umetolewa na na mwandishi wa
kitabu cha “Talk to God” (Ongea na
Mola), Bw. Masija Buchafwe, alipoongea na waandishi wa habari
Jijini Dar es Salaam jana wakati akitambulisha
kitabu hicho.
“Ndani ya vitabu kuna maarifa mengi ambayo ni
msaada mkubwa kwa watu wa rika mbali mbali katika
kukabiliana na changamoto za maisha za kila siku, hivyo itakuwa ni jambo muhimu sana kama taifa
watu wake wakawa na utamaduni wa
kujisomea vitabu. Mimi naweza kuzungumzia Tanzania. Kwa maoni yangu toafauti na miaka ya 1950 hadi
1970 Tanzania ya leo haina
watu wenye kiu ya kusoma vitabu,’’ amesema Bw. Buchafwe.
Amewaomba wazazi na viongozi katika taasisi za
elimu kuwatiamoyo na kuwahimiza vijana kusoma vitabu,
na kueleza kwamba kwa tabia watu wenye
elimu na maarifa ya kisasa ni watu wanasoma sana na watu wasiosoma wana maarifa kidogo ya kileo.
“Kitabu hiki mbali ya kuangazia mambo ya
kiimani lakini pia kimeangazia mambo ya biashara,
siasa, uchumi na upendo ambayo yamekuwa muhimu katika kuchochea maendeleo ya mtu binafsi na Taifa kwa
ujumla,’’ ameeleza Bw. Buchafwe na kusema kwamba
angefurahi kupokea mrejesho
wasomaji wa imani zote.
Bw. Buchafwe amesema kuwa imemchukua takribani
miaka 16 kuandaa na kupata
mchapishaji ambaye ameyaunganisha mashairi na kuwa kitabu cha
kurasa 84.
“Haikuwa kazi rahisi kukamilisha kitabu hiki,
changamoto zilikuwa nyingi lakini nilizitumia katika
kujenga maudhui yaliyobora zaidi kwa faida ya wasomaji,’’ amesema.
Bw. Buchafwe ana Shahada ya Uzamili ya
Mahusiano kwa Umma kutoka Chuo Kikuu cha
Mtakatifu Agustiono (SAUT). Ametafasiri vitabu viwili katika lugha ya Kiswahili kutoka lugha ya
Kingereza: Think Big na God
Sent a Man.
Comments
Post a Comment