BENKI YA MAENDELEO TIB YAUNGA MKONO JITIHADA ZA SERIKALI KATIKA MASUALA YA AFYA
![]() |
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Charles Singili (katikati) akizungumza wakati wa sherehe fupi za kukabidhi misaada kwa Chama cha Watu Wasioona – Wilaya ya Temeke na Taasisi ya Kusaidia Waathirika wa Saratani - TCS HOPE. Wanaomsikiliza ni Mjumbe wa Kamati Tendaji ya TCS HOPE, Bibi Neema Maimu (kushoto ) na Katibu wa Chama cha Watu Wasioona – Wilaya ya Temeke, Bw. Protase Mutakyanga (kulia).
![]() |
| Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Charles Singili (kulia) akikabidhi mfano wa hundi kwa Mjumbe wa Kamati Tendaji ya TCS HOPE, Bibi Neema Maimu kama sehemu ya mchango wa ununuzi wa matiti bandia 2500 kwa wahanga wa saratani ya matiti. |
![]() |
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Charles Singili (kushoto) akikabidhi fimbo nyeupe kwa Katibu wa Chama cha Watu Wasioona – Wilaya ya Temeke, Bw. Protase Mutakyanga (kulia). Katikati ni Meneja Uhusiano na Masoko wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Saidi Mkabakuli.
Na Abdallah Luambano,Dar es salaam
Benki ya
Maendeleo TIB imeunga mkono jitihada za serikali katika kusaidia masuala ya
afya kwa kuwasaidia fimbo nyeupe 86 Chama cha Watu Wasioona – Wilaya ya Temeke
na kutoa jumla ya shilingi 2,500,000 kama sehemu ya mchango wa ununuzi wa
matiti bandia 2500 kwa wahanga wa saratani ya matiti kwa Taasisi ya Kuwasaidia
Waathirika wa Saratani - TCS HOPE.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw.
Charles Singili amesema kwamba TIB kama Taasisi ya Maendeleo inachukulia ustawi
wa wahitaji wenye changamoto za kiafya kama mojawapo ya kichocheo muhimu cha
maendeleo.
Ameongeza
kuwa kwa kutambua umuhimu wa sekta ya afya katika kuleta maendeleo ya nchi,
Benki ya Maendeleo TIB itaendelea kutoa michango hiyo ili kuwasaidia wahitaji
wenye mahitaji maalum ya kiafya pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali
katika masuala ya afya.
Amesema kuwa
kutambua kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, katika kukuza maendeleo
ya sekta ya afya, elimu, utengenezaji ajira na ujasiriamali Benki ya Maendeleo
TIB imejipanga kuendelea kusaidia jitihada hizo kwa kuwekeza katika miradi ya
kimkakati itayosaidia kuongeza kasi ya maendeleo nchini.
“Lengo letu
ni kusaidia jitihada za serikali ili kuongeza kasi ya kufikia malengo ya Dira
ya Taifa ya Maendeleo hususani katika kusaidia nchi yetu kufikia uchumi wa
kipato cha kati ifikapo mwaka 2025” alisema.
Akizungumzia
msaada walioutoa, Bw. Singili alisema kuwa fimbo zilizotolewa ni nyenzo na
visaidizi muhimu kwa wasioona ambavyo zinamsaidia mtu asiyeona aweze kufanya
“Napenda
kuiomba jamii na hasa watumiaji wote wa miundo mbinu ya barabara watembea kwa
miguu, madereva wa magari, pikipiki (daladala/bodaboda) watumiaji wa vyombo
vyote vya moto kuheshimu fimbo nyeupe na kuwasaidia wasioona wawapo
barabarani,” Bw. Singili alitoa wito.
Kwa
upande wake, Katibu wa Chama cha Watu Wasioona – Wilaya ya Temeke, Bw. Protase
Mutakyanga amesema kuwa mchango uliotolewa na Benki hiyo utasaidia wanachama
wake kuweza kuendelea kujishughulisha na masuala ya kujitafutia kipato.
“Mchango
huu utatuwezesha kushiriki shughuli za kimaendeleo hasa zitakazo saidia
kutuingiza kipato,” alisema.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo, Katibu wa Taasisi ya Kuwasaidia Waathirika wa
Saratani - TCS HOPE, Bw. Luca Mabena aliishukuru TIB kwa mchango huo ambao
alisema utasaidia kurejesha furaha kwa kina mama waliothirika na saratani ya
matiti.



Comments
Post a Comment