Kampuni ya TCCIA Investment yapata faida ya milioni 366.57 mwaka 2018
Na Abdalah Luambano, Dar es Salaam
KAMPUNI ya TCCIA Investment Plc imesema jijini Dar es Salaam
kwamba
imepata faida ya shillingi 366.57 milioni kati
ya mwaka 2018 ikilinganishwa
na milioni 246.57 za mwaka 2017 and milioni 154.17 za
mwaka 2016.
“Kampuni yetu inaendelea vizuri”, Mwenyekiti wa Bodi ya
kampuni hiyo, Bw Fortunatus M. Magambo,
ameuambia Mkutano Mkuu wa Mwaka ambao ulifanyika jijini hivi karibuni.
Aliuambia mkutano huo kwamba katika mwaka ulioisha
Desemba 2018, faida ya kampuni kabla ya kodi
ilishuka kwa asilimia 44 hadi 195.78 million ikilinganishwa na faida ya 2017 na kutaja sababu za kushuka
huko kuwa ni pamoja na kupanda kwa gharama
katika manunuzi.
Kisha akawapa habari njema wajumbe kwa kusema kwamba faida baada
ya kodi ilipanda kwa asilimia 49 kufikia
milioni 366.57 kutokana na bidii
iliyofanywa kuchanganua na kusimamia mapato yatokanayo uwekezaji katika hati funani za serikali na pia
gawio kutoka kwa makampuni ambako
TCCIA Investment imewekeza.
Mkutano uliidhinisha malipo ya gawio la shilingi 2.54 kwa
kila hisa kama ilivyokuwa mwaka 2017.
Aidha kampuni hiyo, imewekeza kwenye mashirika na taasisi
mbalimbali za fedha ikiwemo NMB, CRDB, Dar
es Salaam Commercial Bank (DCB), Viwanda
vya Saruji vya TWIGA, SIMBA, Tanzania Breweries (TBL), Swiss Port, na Kiwanda cha Sigara (TCC).
Tangu kuanzishwa kwa kampuni hii mwaka 2005, imeweza kufanya
vizuri
katika uendeshaji wake kiasi cha kuweza kujenga
imani kubwa kwa wanahisa wake hapa
nchini.
Kampuni ya wanahisa ya TCCIA Investment ni moja ya
kampuni za wanahisa inayofanya vizuri na
kuchangia harakati za kuondokana na umasikini
miongoni mwa jamii.
Mwisho.
Mwisho.
Comments
Post a Comment