Waziri Sima aagiza kulindwa chanzo cha mto Luegu wilayani Namtumbo


Na Mwandishi Wetu, Namtumbo
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),
Bw. Musa Sima  ameagiza kulindwa na kutunzwa kwa chanzo cha Mto Luegu
kilichopo kwenye Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma  ambacho maji yake
husambazwa  katika mikoa 11 na wilaya 32 kwa kutovamiwa na wakulima.


Akikagua  chanzo hicho cha maji kilichopo kwenye Kijiji cha Ngwinde
wilayani hapa,  Naibu Waziri Sima ambacho maji yake  yanaigia Mto
Rufiji ambako kunatarajiwa kujengwa bwawa kubwa la kuzalisha umeme wa
maji  kiasi cha megawati 2,100 wa Stiegler’s Gorge.


“Chanzo hiki cha maji kinategemewa pia kuongeza uzalizaji wa umeme
katika vituo vya Kidatu, Lipera na Kihansi pia,” alisema na kuwaomba
wananchi wanaoishi  karibu na eneo hilo kulinda chanzo hicho muhimu
nguvu zote.


Bw. Sima ambaye katika ziara hiyo alitanguzana pia na maofisa
waandamizi kutoka Baraza la Kuhifadhi Mazingira nchini (NEMC) ametoa
pia angalizo kwa uongozi wa wilaya kuwa makini na wakulima na wafugaji
kwani  eneo hilo lilivyo linawavutia kutokana na ubichi wake.


Alisema chanzo cha maji ya Mto Luegu ni muhimu sana kwa uzalishaji wa
umeme hapa nchini na hivyo utunzwaji wake utawezesha watanzania  wengi
 kupata umeme kwa bei rahisi hivyo lazima hatua za makusudi
zichukuliwe kuutunza.


Kwa upande wake, Afisa Mifugo wa Wilaya ya Namtumbo, Bw.Kelvin Mnali
alimhakikishiwa Waziri Sima kuwa uongozi wa wilaya umeelekeza nguvu
zake katika eneo hilo na wananchi wanatambua umuhimu mkubwa wa chanzo
hicho cha maji kwa ustawi wa maisha yao.


“Mto Luegu ni mkombozi mkubwa kwa wakazi eneo hili na wao wenyewe pia
wamekuwa walinzi wa kutunza chanzo hiki ambacho maji yake yanategemewa
na maeneo mbalimbali hapa nchini,” Bw. Mnali alisema.


Alisema wananchi wamekuwa wakijihusisha na shughuli za kilimo mbali na
eneo la chanzo mto huo kwa maji yake hutumika katika matumizi
mbalimbali.


 “Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli
inahimiza suala la utunzaji mazingira ambapo kila mtanzania anawajibu
wa kuyatunza ili yawezekumsaidia,” alisema na kuongeza kuwa serikali
haitamvulia mtu yeyote anayeharibu mazingira.


Bw Sima yupo katika ziara ya kutembelea mikoa ya Lindi, Mtwara,
Ruvuma, Njombe, Mbeya Iringa na Morogoro kujifunza changamoto za
kulinda mazingira na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu. Jana alitarajiwa
kutembelea Mkoa wa Njombe.
Mwisho.


Comments

Popular posts from this blog

Tanzania praised for being keen on fertilisers going to farmers

Gold mine in Songwe wins ministerial praise for protecting environment

NEMC warns on emptying effluent in built-up areas, flood waters