UDOM, Shell Tanzania Semina kwa wahitimu vyuo vikuu yawavuta wengi
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
WASHIRI kwenye warsha ya kuwaandaa vijana na maisha mara wamalizapo masomo yao ya shahada ili waweze kwenda sambamba na soko la ajira wameipongeza Shell Tanzania kwa udhamini kwani imewajengea uwezo mkubwa.
Mafunzo hayo yametolewa Chuo Kikuu Dodoma ambapo wajasiriamali na wasomi wa kada mbalimbali waliwasilisha mada ili kuwapa vijana msukumo
wa kupambana na soko la ajira ndani na nje ya
Tanzania.
Akizungumza wakati wa semina hiyo iliyofanyika mwishoni mwa juma Kaimu Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Ardhi, Dkt. Godlisten Kombe aliwashukuru
kampuni ya Shell Tanzania kwa namna inavyosaidia
jamii katika Nyanja mbalimbali ikiwemo
elimu.
“Tunawashukuru sana wenzetu wa Shell Tanzania kwa kujitoa kwao katika kusaidia jamii za watanzania, kwa kipekee kabisa ni kwa namna walivyoitikia mwaliko wetu ili pamoja nasi
kuweza kuandaa warsha hii hapa UDOM
katika Ndaki ya Sayansi na Ardhi, “ alisema Dkt Kombe.
Aidha Dkt Kombe amesema kuwa mafunzo haya yamekuja katika wakati muafaka ili kuwajenga wanafunzi na hasa tunapoelekea uchumi wa kati na
wa viwanda ifikapo 2025.
“Jitihada hizi zina maana kubwa sana kwetu kama Chuo na Taifa kwa ujumla kwa kuwa inawafanya vijana wawe na chachu ya kutafuta na kufanya kazi kwa bidii na hivyo kuifanya sera ya
uchumi wa kati na viwanda viweze kufikiwa
kwa urahisi.” Alisisitiza Dkt Kombe
Katika hatua nyingine Dkt Kombe alitumia nafasi hiyo kuto wito kwa taasisi na kampuni mbalimbali nchini zinajitokeza katika kuwasaidia
watanzania katika nyanja mbalimbali kama ambavyo
Shell Tanzania wanafanya.
“Nitoe wito kwaMakampuni mbalimbali kujitokeza katika kuwasaidia vijana katika kuwajengea uwezo na hatimae tukapata nguvu kazi ya kuzalisha katika sekta mbalimbali kama ambavyo Shell
Tanzania wameguswa kwa vijana wa hapa
Udom, ni matumaini yangu kuwa semina hii
itawabadilisha vijana.” Alisema Dkt Kombe
itawabadilisha vijana.” Alisema Dkt Kombe
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Oxford Policy Management Tanzania (OPM), Dkt Charles Sokile aliwaasa vijana kutumia nafasi mbalimbali
wanazozipata katika kujijengea uwezo ikiwemo
semina hii iliyoandaliwa na Shell
Tanzania kwa kuwa kuwa soko la ajira linaushindani mkubwa.
“Vijana lazima wajifunze namna ya kujiongezea thamani itakayowafanya wapenye katika soko la ajira ambalo kwa sasa limekuwa na ushindani mkubwa, na njia mojawapo ni hii ambayo Shell wamewaonyesha lakini mbali na hii zipo nyingi huko mitaani, ni jukumu lao kuzitumia kwa
lengo la kufikia malengo yao ambayo wanakuwanayo wanapokuwa vyuoni,” alisema Dkt Sokile
“Vijana lazima wajifunze namna ya kujiongezea thamani itakayowafanya wapenye katika soko la ajira ambalo kwa sasa limekuwa na ushindani mkubwa, na njia mojawapo ni hii ambayo Shell wamewaonyesha lakini mbali na hii zipo nyingi huko mitaani, ni jukumu lao kuzitumia kwa
lengo la kufikia malengo yao ambayo wanakuwanayo wanapokuwa vyuoni,” alisema Dkt Sokile
Pia aliwataka vijana kutokuwa na aibu wakati wakiwa katika mwelekeo wa kutafuta mafanikio ambayo wamekuwa wakiyaota tangu wakiwa wadogo.
“Vijana wetu wamekuwa na changamoto nyingi katika soko la ajira lakini changamoto hizo baadhi zinatengenezwa na vijana wenyewe kwa kupuuza
mambo ambayo wangekuwa na ujasiri wa kuyafanya
wangefika mbali, hivyo lazima wawe na
uthubutu,” alisema Dkt Sokile.
Simon Jackson ambaye ni Mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika fani ya Uchenjuaji na uchakataji wa madini aliwashukuru kampuni ya Shell Tanzania kwa namna ambavyo waendaa semina hiyo kwani
wao kama walengwa imewaongezea thamani
kubwa.
“Tunawashukuru Shell Tanzani kwa kuwa semina hii imekuwa muhimu sana kwetu kwa kutuongezea thamani lakini muhimu zaidi ni kwa namna ilivyokutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta
tofauti,” alisema Bwana Jackson na kutoa
wito kwa kampuni na taasisi zingine kuiga mfano wa Shell Tanzania.
Afisa Utafiti na Uzalishaji kutoka Shell Tanzania, Bw. Marcus Luoga alieleza kufurahishwa kwake na mwaliko wa Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
na Shell Tanzania walitumia nafasi hiyo
kuwaleta wataalam mbalimbali kwa lengo la
kueleza vijana njia za kupita ili kufikia malengo yao.
“Tunaushukuru uongozi wa Chuo Kikuu Dodoma hususani ndaki ya sayansi za ardhi kwa namna walivyoona mchango wa Shell Tanzania na hivyo kutualika katika tukio hili muhimu. Shell Tanzania
tumewaalika wataalamu mbalimbali ili
kuelezea namna nzuri inayoweza kuwasaidia wahitimu
wa vyuo vikuu kufikia malengo yao.” Alisema bwana Luoga
Kampuni ya Shell inafanya kazi katika mataifa matano ambayo ni Uingereza, Australia, Malasia, Marekani na Tanzania ambapo imekuwa
ikitoa michango mbalimbali kwa jamii ili
kuondokana na changamoto za maisha.
MWISHO.
Comments
Post a Comment