Waziri Bashe azindua kiwanda cha pamba cha Chato

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB),Bw.Japhet Justine (kushoto)akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Kilimo,Bw.Hussein Bashe muda mfupi baada ya kukizindua kiwanda cha pamba cha Chato(CCU) mwishoni mwa wiki.Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Gabriel.TADB imeshatoa kiasi cha shilingi bilioni 6.7 kukifufua kiwanda hicho.


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania(TADB),Japhet Justine akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha pamba Chato mwishoni mwa wiki.TADB imetoa kiasi cha shilingi bilioni 6.7 kukifufa kiwanda hicho.Uzinduzi ulifanywa na Naibu wa Kilimo,Bw. Hussein Bashe na kuhudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Gabriel.

 

Na Abdallah Luambano, Chato

NAIBU Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amezidua Kiwanda cha Pamba cha Chato (CCU) na kuielezea hatua kama mpango kabambe wa serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais  Dkt. John Pombe Magufuli  wa kujenga sekta ya kilimo inayojitegemea sambamba na uhakika wa upatikanaji wa malighafi.

Akizungumza mara baada ya kukizinduzi wa Kiwanda cha Pamba cha Chato (CCU) mwishoni mwa wiki, Waziri Bashe alisema kufufuliwa kwa kiwanda hicho mwanzo mzuri kwa wakulima pamba kuongoza uzalishaji na kuinua vipato vyao.

“Mradi wa kufufua kiwanda hiki  umegharimu jumla ya shilingi 6,714,804,447 kutoka katika benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) lengo likiwa kuimarisha sekta ya kilimo ili kuwanufaisha wakulima wa pamba,’’ alisema  Bw.Bashe huku akishangiliwa.

Alisema kufufuliwa kwa kiwanda hicho ambacho kilisimama kufanya uzalishaji kwa miaka kadhaa kutawafanya wakulima wilayani Chato na maeneo mengine ya jirani kuongeza uzalishaji na hivyo kuleta unafuu wa maisha kwa wakulima.

 “Serikali imedhamiria kuifanya sekta ya kilimo inajitegemea kwa kuwa mbali ya kutoa ajira kwa watanzania walio wengi lakini pia imekuwa na mchango wa asilimia 25 katika pato la Taifa,’’ alisema.

Aidha, waziri Bashe  aliipongeza Benki ya Kilimo kwa jitihada zake za kuwaletea wakulima maendeleo kwa kuwapa mikopo yenye mashrti nafuu jambo ambalo linaongeza tija katika ukuaji wa uchumi wa Nchi.

“Natoa pongezi kwa TADB, Wizara, wadau wa kilimo pamoja na chama cha ushirika wilayani chato (CCU) kwa namna tulivyoshirikiana kuhakikisha kiwanda hiki kinaendelea na uzalishaji na hivyo kuchochea uzalishaji wa zao la pamba,’’ alisema na kuziomba taasisi zingine za fedha
kujitokeza na kuwekeza katika sekta ya kilimo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Japhet Justine alisema kuzinduliwa kwa kiwanda hicho kutaongeza thamani ya zao la pamba ambayo ilishuka tangu msimu wa 2013/14.

“Tunaamini hatua tunazochukua kwa mazao ya kimkakati ikiwemo zao la pamba iyasaidia katika kuongeza thamani yake na hivyo kuwa na bei ambayo itamfanya mkulima anufaike zaidi na kuchungia ukuaji wa pato la Taifa,’’ alisema.

Alisema bei ya msimu huu imekuwa nzuri ukilinganisha na misimu kadhaa ya hapo awali na kwamba wataendelea kuimarisha upatikanaji wa soko zuri na lenye faida kwa mkulima.

“Msimu unaomalizika tulijitahidi kununua pamba kwa wakulima kwa bei ambayo waliifurahia lakini tunaendelea kuweka mikakati ya kulifanya zao la pamba kuwa na faida zaidi kwa kufufua viwanda vya kuchakata pamba kama hiki cha Chato,’’ alisema Bashe.

Naye Mmoja wa viongozi  wa Chama cha Msingi wilayani humo ambaye jinalake alikupatikana mara moja , mbali ya kuishukuru benki ya kilimo alisema kufufuliwa kwa kiwanda hicho kutaongeza ajira kwa watanzania.

“Kufufuliwa kwa kiwanda hiki kutaleta manufaa makubwa kwa wananchi wa Chato kwani wataongeza kipato chao na kumudu gharama za maisha na pia kuongeza ajira za moja kwa moja kiwandani,’’ alisema.

Kiwanda hicho kitanufaisha Vyama vya Ushirika wa kilimo na Masoko (AMCOS) 52 vyenye jumla ya wakulima 7000 kutoka Chato, Biharamulo na Muleba.

Comments

Popular posts from this blog

Set aside land for investment, Kairuki tells RCs,district councils

Mkuu wa Mkoa Pwani asifu juhudi za mmiliki wa Makampuni ya Global Packaging na Wande Printing

17 projects to house 80,000 tonnes of crops being built