Mkutano mkuu TPSF kutathmini muundo, utendaji wake
Mkutano mkuu TPSF kutathmini muundo, utendaji wake Daniel Lwimiko, Dar es salaam MAANDALIZI ya Mkutano Mkuu wa 19 wa Mwaka (AGM) wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) unaotarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam kesho yamekamilika ambapo wanachama wameombwa kushiriki kwa wingi pamoja nakufanya tathmini ya utendaji na kuangalia muundo wake ili kuendana na wakati. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Bw. Godfrey Simbeye alisema wajumbe watapata nafasi kujadiliana masuala mbalimbali ikiwemo muundo wa taasisi ili kukidhi matarajio ya wadau wote katika sekta za biashara na uchumi. “Mkutao huo wa siku moja umelenga kupitia upya muundo wa TPSF na namna ya kuwafikia wanachama wapya ili kwenda sambamba na azma ya serikali ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kujenga uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025,” alisema Bw. Simbeye. Alisema TPSF kama taasisi inayosimamia